NA MWANDISHI WETU
MKUU
wa Wilaya ya Kusini, Mheshimiwa Rajab Yussuf Mkasaba amewahimiza
Masheha wa Wilaya ya Kusini kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wao juu ya
kufuata sheria na misingi ya haki za binaadamu na utawala bora kwa azma
ya kuwawezesha kutekeleza vyema majukumu yao.
Mkasaba
ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya haki za
binaadamu na utawala bora yaliyowashirikisha Masheha wa Wilaya hiyo
ambayo yalitayarishwa na Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora
yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kusini, Kitogani.
Katika
maelezo yake mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza Masheha kuhakikisha
wanapokea vyama mafunzo hayo ili hatimae wakayafanyie kazi katika jamii
na kuwa mabalozi juu ya utekelezaji wa mafunzo hayo.
Amesema
kuwa, bado kuna baadhi ya wananchi katika jamii hawajapata uelewa juu
ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora hivyo, elimu hiyo itasaidia kwa
kiasi kikubwa kufikia lengo lililokusudiwa na Tume ya Haki za Binaadamu
na Utawala Bora la kuiwezesha jamii kuwa na ueleza juu ya dhana hiyo.
Aliongeza
kuwa dhana ya Utawala Bora ikitekelezwa huleta faida kadhaa ikiwemo
matumizi mazuri ya rasilimali za nchi, maendeleo endelevu, kupungua kwa
umasikini, ujinga na madhadhi, kutokomea kwa rushwa, kuimarika kwa
huduma bora za jamii, kuimarika kwa amani na utulivu, kuheshimiwa kwa
haki za binaadamu, utatuzi wa migogoro pamoja na kuleta ustawi wa
wananchi.
Aidha,
Mkuu wa Wilaya hiyo alieleza kwamba miongoni mwa vyanzo vya Haki za
Binaadamu nchini Tanzania ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977 amba pia, vipo vyanzo vingine vya haki za binaadamu nchini
kama vile Sheria mbali mbali zilizopo.
Mkuu
huyo wa Wilaya alisema kuwa Utawala Bora na Haki za Binaadamu ni mambo
yanayokwenda kwa pamoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba ukiukwaji wa
misingi ya utawala bora unasababisha uvunjaji wa haki za binaadamu na
uzingatiaji wa misingi ya utawala bora unasaidia ulinzi na hifadhi ya
haki za binadamu.
Alisisitiza
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zamzibar chini ya uongozi wa Rais Dk.
Mwinyi imeendelea kutekeleza wajibu wa kulinda haki za binaadamu na watu
wake wka kutekeleza Sheria, Sera, Mipango, Mikakati na programu
zinazotafsiri upatikanaji wa haki za mbali mbali.
Sambamba
na hayo, utayari wa Serikali kwa kuwa na chombo kama Tume ya Haki za
Binaadamu na Utawala Bora kinachopima na kuishauri Serikali kwenye
utendaji kazi wa kulinda na kukuza haki za binaadamu ambapo ni ushahidi
kuwa Tanzania ni nchi inayothamini demokrasia na kuwa ina Serikali
inayowajibika vyema kwa wananchi.
“Katika
kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Rais Dk.
Mwinyi na Awamu ya Sita ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan hali ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora
zimeimarika na Tume imetekeleza vyema majukumu yake kwa uhuru”,alisema
Mkasaba.
Nae
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Juma
Msafiri Karibona alisema kuwa wananchi wanapaswa kujua Haki za
Binaadamu na Utawala Bora kupitia kwa Masheha ili waweze kutambua wajibu
wao katika harakati zao za kimaisha.
0 Comments