NA MUNIR SHEMWETA-WANMM
KAYA
255 za vijiji vitatu vya Igeleke, Usokami na Kibengu vilivyopo
Halmasauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa zitaondolewa eneo la
Hifadhi ya Shamba la Sao Hill.
Sehemu
ya wananchi wa Kijiji cha Kibengu katika Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara na Kamati ya Mawaziri
Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi
katika vijiji 975.
Uamuzi
huo umetangazwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt
Angeline Mabula Oktoba 26, 2022 wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara
za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji
975 ilipotembelea na kukutana na wananchi wa Kijiji cha Kibengu
kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Dkt.Mabula
alisema, uamuzi unaofanywa kuhusiana na eneo hilo una nia njema kwa
mustakabali wa taifa na vizazi vijavyo kwa kuwa kaya hizo zimekuwa
zikifanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ikiwemo kilimo cha
mazao ya kudumu na mazao ya msimu na kuharibu mazingira.
Alitaja
idadi ya kaya kwa kila kijiji kuwa, ni kaya nne za Kijiji cha Igeleke
kinachohusisha vitongoji vya Kihesa, Mdodi, Lwombogole na Igangilonga.
Kaya
nyingine ni 97 za Kijiji cha Usokami zilizoko vitongoji vya Kidete,
Msega, Mgwao, Ilamba, Nyamifwa na Uhwana pamoja na kaya 154 za kijiji
cha Kibengu ambazo zote zitatakiwa kuondoka.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt.Angeline Mabula
akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Kibengu katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa wakati Kamati ya Mawaziri Nane
inayoshughulikia migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975
ilipotembelea kijiji hicho kilichopo Hifadhi ya Shamba la Sao hill.
“Hiyo
ni takwimu za kaya zinazoenda kuathirika na siyo kuhama eneo moja
kwenda lingine lakini kwa utaratibu maalum na hakuna atakaye kuja kusema
ondokeni leo,” alisema Dkt. Mabula.
“Mheshimiwa
Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan)
amesema hamtaondoka bure na uthamini itafanyika kwa yoyote aliyetimiza
masharti na kwa kuwa kijiji kimeandikishwa maana yake mmekidhi vigezo
vya kulipwa, na kila mlichowekeza katika eneo husika hakuna
atakayedhurika,”alisema.
Baadhi
ya mapendekezo ya wataalamu kuhusiana kaya zinazotakiwa kuondoka eneo
la hifadhi ya msitu wa Sao Hill mkoani Iringa ni pamoja na kuwekwa ukomo
kwa wananchi kuondoa miti ndani ya hifadhi sambamba na hifadhi kutoa
notsi ya kisheria kwa wananchi kuondoa miti yao kabla ya tarehe ya
ukomo.
Mkoa
wa Iringa unahusisha vijiji na mitaa 15 yenye migogoro ya matumizi ya
ardhi ambapo vijiji hivyo vimeainishwa katika sehemu kuu sita kulingana
na aina ya mgogoro na uamuzi uliotolewa na Baraza la Mawaziri.
Manaibu
Mawaziri wa Wizara za Kisekta waliopo katika ziara hiyo kila mmoja
alielezea umuhimu wa sekta yake katika kulinda na kuimarisha rasilimali
za nchi kupitia sekta ya ardhi.
Khamis
Hamza Chilo mbali na kupongeza upandaji miti ya biashara wilayani
Mufindi alishauri wananchi kupanda miti ya kudumu ili kurithisha vizazi
vijavyo.
‘’Nasema
haya kwa sababu Tanzania kwa sasa inalia na kuathirika kwa mabadiliko
ya tabia nchi na tuchukue tahadhari na kujitahidi kwa kutunza mazingira
na kupanda miti ili mwisho wa siku tusilete athari kwa viumbe
hai,"alisema Chillo.
0 Comments