NA MUNIR SHEMWETA-WANMM
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
ameridhia wananchi wa Kitongoji cha Ikanka kilichopo Kijiji cha Itumba
Wilaya ya Ileje kuendelea kuishi sehemu ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa
Ileje Range mkoani Songwe.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifurahi na
wananchi wa kitongoji cha Ikanka katika kijiji Itumba wilayani Ileje
wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia
migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975 ilipotembelea kitongoji
hicho jana.
Uamuzi
huo unakifanya Kitongoji cha Nkanka sasa kutambuliwa ndani ya Hifadhi
ya Msitu wa Ileje Range kutokana na idadi ya kaya 105 zenye makazi
zilizopo ndani ya eneo.
Aidha,
uamuzi huo pia umegusia mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi za
msitu wa Mugombezi uliopo Kijiji cha Nyimbili katika Kata ya Mlowo,
Ilengo Mbozi mkoani Songwe.
Akitangaza
uamuzi huo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.
Dkt.Angeline Mabula amesema sehemu ya eneo la hifadhi ekari 278
zitamegwa na kubaki kwa wananchi kutoka ekari 414 kwa kuwa eneo hilo
limeendelezwa kwa shighuli za kilimo, makazi na kuwekwa huduma za
kijamii kama uwanja wa mpira na pampu ya maji.
Waziri
Mabula amewatahadharisha wananchi walioruhusiwa kuendelea eneo hilo
kutojaribu kuongeza maeneo wanayoishi huku akieleleza kuwa, mara baada
ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kukamilika maeneo yote ya
hifadhi yanatakiwa kulindwa.
Aidha,
Dkt.Mabula ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikanka
Oktoba 24, 2022 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za
Kisekta aliagiza shughuli za kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji nazo
zisitishwe ili kunusuru vyanzo vya maji ndani ya hifadhi.
Naibu Waziri wa Kilimo Athony Mavunde,akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kitongoji cha Ikanka Ileje Songwe.
Kwa
upande wao Mawaziri walioambatana na Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi walisisitiza umuhimu wa kutunzwa mazingira pamoja na
kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi kwa maeneo yote yaliyomegwa.
Naibu
waziri wa Maji, Meryprisca Mahundi aliwaambia wananchi wa Kitongoji cha
Ikanka kuwa, baada ya kuruhusiwa kuendelea kuishi eneo hilo wahakikishe
wanatunza na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuepuka shughuli zozote
zitakazosababisha uharibifu wa vyanzo hivyo.
Khamis
Hamza Chilo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
alisisitiza suala la wananchi kupanda miti katika maeneo waliyoachiwa
ili kutunza mazingira.
Naibu Waziri wa Kilimo Athony Mavunde,akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kitongoji cha Ikanka Ileje Songwe.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde pamoja na Naibu Waziri Mifugo na
Uvuvi , Abdallah Ulega walieleza umuhimu wa maeneo yaliyomegwa kupangiwa
matumizi ya ardhi na kupimwa sambamba na kuanishwaa maeneo ya kilimo,
mifugo pamoja na uvuvi ili kuepuka kutengeneza migogoro mingine.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano na wananchi wa Ikanka Ileje Songwe jana.
Katika
hatua nyingine, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Dkt.Angeline Mabula amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kuhakikisha
wanatekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri kuhusiana na migogoro ya
matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwa kuweka mpango wa utekelezaji
hasa kwa yale maeneo ambayo hayana tathmini ya kina.
Katika
maamuzi yake, Baraza la Mawaziri liliamua vijiji 920 kati ya 975 vyenye
migogoro katika ranchi, mapori ya akiba, mashamba na vyanzo vya maji
kubaki ingawa baadhi ya vijiji vitahusisha marekebisho ya mipaka kwa
njia shirikishi,
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Dkt Angeline Mabula
akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Ikanka katika Kijiji Itumba
wilayani Ileje wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta
inayoshughulikia migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975
ilipotembelea kitongoji hicho.(Picha na WANMM).
Hata
hivyo, vijiji 55 kati ya 975 vinaendelea kufanyiwa tathmini na kamati
na wataalamu wake kutoa mapendekezo kwa ajili ya maamuzi.
Tayari
kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta imeshatembelea mikoa kumi
na tisa kati 26 kamati imeshapeleka mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la
Mawaziri na inaendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa,
Njombe na Ruvuma.
0 Comments