NA MWANDISHI WETU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Korea
imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika
ujenzi wa chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) nchini
Tanzania.
Mheshimiwa
Majaliwa amesema kuwa lengo la chuo hicho ni kuwasaidia vijana
kuendeleza ubunifu wao na kuonesha namna wanavyoweza kuunda vifaa
mbalimbali “Mpango wa Rais wetu wa kuwapa vijana shughuli za kufanya
katika eneo la Sayansi na Teknolojia ni mpango ambao unaungwa mkono na
Serikali ya Korea”.
Waziri
Mkuu amesema hayo Oktoba 27, 2022 baada ya kumaliza
mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Han Duck-Soo
katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu uliopo Seoul.
Oktoba
14, 2021 Mheshimiwa Rais Samia akizungumza katika kilele cha Mbio za
Mwenge kitaifa kwenye Viwanja vya Magufuli, Wilayani Chato, Mkoani
Geita, alisema Serikali inatarajia kujenga chuo bora zaidi cha kisasa
cha TEHAMA ili kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi katika matumizi ya
teknolojia hiyo.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Mirae
Chemical ambao wanajenga kiwanda cha kuchakata maganda ya korosho baada
ya kubanguliwa ambacho kwa mara ya kwanza teknolojia hiyo inaingia
nchini Tanzania.
“Hii
ni fursa kubwa kwa wakulima wetu, hiki kilikuwa ni kilio kikubwa kwa
wakulima, tumezungumza nao na kuwasisitiza waendelee na ujenzi katika
eneo la Mkuranga. Kiwanda hiki kitakuwa kinakusanya maganda ya korosho
kwa wakulima, hii ni fursa kwa wakulima kwani itaongeza tahamani ya zao
hilo.”
Amesema
kuwa kwa sasa Serikali itahamaisha Halmashauri nchini kutafuta maghala
kwa ajili ya kukusanya maganda ya korosho yaliyonunuliwa kutoka kwa
wakulima. “Wakulima sasa wajipange kuuza maganda ya korosho, kwasasa
ubanguaji utafanyika ndani ya nchi na wakulima wataanza kuuza maganda
pamoja na mbegu inayopatikana kwenye zao la korosho.
0 Comments