NA MUNIR SHEMWETA-WANMM
WAZIRI
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula ametaka
maeneo ya yanayomegwa kwa ajili ya kupatiwa wananchi waliovamia hifadhi
yapangiwe mpango wa matumizi ya ardhi na kutolewa hati kwa wamiliki
wake.
Dkt.Mabula
alitoa kauli hiyo Oktoba 27, 2022 katika Kijiji cha Mpanga kilichopo
Wilaya ya Wanging'ombe wakati timu ya mawaziri nane wa wizara za kisekta
inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975
ilipotembelea mkoa wa Njombe ikiwa ni mfululizo wa ziara zake kawenye
mikoa ya Tanzania Bara.
Kijiji
cha Mpanga ni moja ya vijiji 11 vilivyopo wilaya ya Wanging'ombe na
Makete mkoani Njombe ambavyo vimemegewa eneo kutoka Hifadhi ya Pori la
Akiba la Mpanga Kipengele.
Dkt.Mabula
alisema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeridhia baadhi ya vijiji
kwenye mkoa wa Njombe kubaki maeneo ya hifadhi za Mapori ya Akiba ingawa
wananchi wake waliingia bila ridhaa ya Serikali.
Kwa
mujibu wa Dkt.Mabula, ili kuondokana na migogoro ya ardhi vijiji
vilivyomegewa maeneo vitapimwa na kumilikishwa ili wamiliki kujua mipaka
sambamba na kuweza kutumia hati kukopa fedha benki na fedha kutumika
kuboresha shamba au mifugo.
"Kinachofanyika hapa siyo tu kutoa maeneo, eneo linatolewa lakini liwekewe mpango mzuri na endelevu ili kuona jinsi gani mnaweza kutumia ardhi mliyopewa kwa faida na kwa sababu tunaongezeka basi mpango uwe mzuri na endelevu,"alisema Dkt.Mabula.
Amebainisha
kuwa, ni lazima maeneo yanayopangwa yaanishwe matumizi yake kama vile
maeneo ya akiba, hifadhi, makazi na uwekezaji na kutaka wakati wa
utekelezaji wataalamu wazingatie mpango wa matumizi katika maeneo hayo.
Timu ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ambayo inashughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975 imemaliza ziara yake katika mkoa wa Njombe ukiwa ni mkoa wa 22 kati ya 26 ya Tanzania Bara na inaendelea na ziara yake katika mkoa wa Ruvuma.
0 Comments