NA MUNIR SHEMWETA-WANMM
WAZIRI
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula ametaka
maeneo ya yanayomegwa kwa ajili ya kupatiwa wananchi waliovamia hifadhi
yapangiwe mpango wa matumizi ya ardhi na kutolewa hati kwa wamiliki
wake.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (kushoto),
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (wa pili kushoto) na Naibu
Waziri Maliasili na Utalii, Mery Masanja wakicheza na bibi aliyekuwa
akifurahia maamuzi ya Serikali kukibakisha Kijiji cha Mpanga kilichokuwa
kwenye Hifadhi ya Mpanga Kipengele wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa
Wizara za Kisekta ilipotembelea kijiji hicho mkoani Njombe Oktoba 27,
2022.
Dkt.Mabula
alitoa kauli hiyo Oktoba 27, 2022 katika Kijiji cha Mpanga kilichopo
Wilaya ya Wanging'ombe wakati timu ya mawaziri nane wa wizara za kisekta
inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975
ilipotembelea mkoa wa Njombe ikiwa ni mfululizo wa ziara zake kawenye
mikoa ya Tanzania Bara.
Kijiji
cha Mpanga ni moja ya vijiji 11 vilivyopo wilaya ya Wanging'ombe na
Makete mkoani Njombe ambavyo vimemegewa eneo kutoka Hifadhi ya Pori la
Akiba la Mpanga Kipengele.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akizungumza
katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Mpanga wilayani
Wanging’ombe wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta
ilipotembelea kijiji hicho mkoani Njombe Oktoba 27, 2022.
Dkt.Mabula
alisema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeridhia baadhi ya vijiji
kwenye mkoa wa Njombe kubaki maeneo ya hifadhi za Mapori ya Akiba ingawa
wananchi wake waliingia bila ridhaa ya Serikali.
Kwa
mujibu wa Dkt.Mabula, ili kuondokana na migogoro ya ardhi vijiji
vilivyomegewa maeneo vitapimwa na kumilikishwa ili wamiliki kujua mipaka
sambamba na kuweza kutumia hati kukopa fedha benki na fedha kutumika
kuboresha shamba au mifugo.
Naibu
Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Anthony Mtaka (kulia) wakimsiliza Bi.Neema (kushoto) ambaye ni mkulima
wa mahindi na mkazi wa Kijiji cha Mpanga Wilaya ya Wanging’ombe wakati
Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipotembelea kijiji hicho
mkoani Njombe Oktoba 27, 2022.
"Kinachofanyika hapa siyo tu kutoa maeneo, eneo linatolewa lakini liwekewe mpango mzuri na endelevu ili kuona jinsi gani mnaweza kutumia ardhi mliyopewa kwa faida na kwa sababu tunaongezeka basi mpango uwe mzuri na endelevu,"alisema Dkt.Mabula.
Amebainisha
kuwa, ni lazima maeneo yanayopangwa yaanishwe matumizi yake kama vile
maeneo ya akiba, hifadhi, makazi na uwekezaji na kutaka wakati wa
utekelezaji wataalamu wazingatie mpango wa matumizi katika maeneo hayo.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisisitiza jambo mbele ya
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa
Wizara za Kisekta ilipowasili ofisi ya Mkuu wa mkoa Njombe Oktoba 27,
2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
Timu ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ambayo inashughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975 imemaliza ziara yake katika mkoa wa Njombe ukiwa ni mkoa wa 22 kati ya 26 ya Tanzania Bara na inaendelea na ziara yake katika mkoa wa Ruvuma.
0 Comments