NA MUNIR SHEMWETA-WANMM
NAIBU
Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameonya wale wote
wanaochepusha maji kwa ajili ya kufanya shughuli zao ikiwemo kumwagia
mashamba na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Naibu
Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa na Mawaziri
wenzake wa wizara za kisekta wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji
Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022. (PICHA NA
WIZARA YA ARDHI).
Amesema
hayo Oktoba 27, 2022 wakati kamati ua mawaziri nane wa wizara za
kisekta za kushughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi ilipokwenda
kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpanga katika Halmashauri ya Wilaya
ya Wanging,’ombe mkoani Njombe.
Amewataka
wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza maeneo maji yanapoanzia na
kufuata sheria pale wanapotaka kutumia na kusisitiza wanaochepusha maji
kiholea waache kuacha mara moja.
‘’Kuna
utaratibu na siyo kama nazuia maji yasitume, lakini kuna Bodi ya Maji
ya Mto Rufiji inafanya kazi vizuri na kuna taratibu zake ukitaka
kumwagilia maji nenda ofisi zao na unapewa utaratibu na unakuwa
mtanzania mzalendo.
“Wewe
unayelima na kumwagia mazao yako ufanikiwe basi usiwe kikwazo kwa
watumiaji wengine wa maji majumbani kwa sababu ukitaka kuyavuta yote
shambani kesho yake mradi, majengo makubwa na usambazaji mabomba yenye
thamani ya mabilionji ya fedha itakwama, wewe unachepusha maji kwenye
chanzo yatafikaje kwenye matenki tuache kuchepusha maji,"alisema
Maryprisca.
Aidha,
alionya wananchi wanaolima ‘vinyungu’ kwenye vyanzo vya maji kuacha
tabia hiyo na kueleza kuwa, mtu yeyote anayelima maeneo ya vyanzo maji
ni adui namba moja wa zile jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa
sababu anasababisha maji kukauka na kusababisha miundo mbinu inayotolewa
kwa ajili ya miradi ya maji kukosa thamani.
Kwa
mujibu wa Maryprisca, shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ni
mwiko na haviruhusiwi kwa kuwa zinasababisha maji kukauka huku lengo la
serikali kupitia wizara yake likiwa kuendelea kupata maji zafi na
salama.
Pia
Naibu wa Waziri wa Maji aliwataka wananchi kulinda na kutunza vyanzo
vya maji na kuacha kabisa kufanya shughuli zozote za kibinadanamu kwa
kuwa zinaweza kuharibu vyanzo hivyo alivyovieleza vinahitaji uoto wa
asili ili viweze kuimarika.
0 Comments