NA ADELADIUS MAKWEGA
WAKRISTO
wameambiwa kuwa kila wanapokwenda kanisani wanaabudu,
wanasali,wanasikiliza neno la Mungu na kuomba msamaha ili kupata neema
ya Mungu na vile vile wanakwenda kufahamu mambo yanayompendeza Mungu,
kumshukuru Mungu kwa yale mema anayotenda katika maisha yetu yao.
Hayo
yamesemwa na Padri Novatus Mrema, Paroko wa Parokia ya Mbagala
Kizuiani, Kanisa wa Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, Jimbo Kuu Katoliki
la Dar es Salaam, wakati wa misa ya kwanza ya Jumapili ya 30 ya mwaka C,
Oktoba 23, 2022.
Akiendelea
kuhubiri Padri Mrema amesema kuwa, kila mara mkristo anapokwenda kusali
anahimizwa na masomo ya jumapili hii juu ya toba.
“Je
sala zako zinafanana na ya mfarisayo au zinafanana na ya mtoza ushuru?
Mfano huo ni sawa na kioo kilicho mbele yetu, ili tuweze kujiona.”
Ameongeza kuwa, si vizuri kujiona wewe ni mwenye haki zaidi ya mwingine, mbele ya Mungu tuyaone madhaifu yetu na kujinyenyekeza.
Misa
hiyo pia ilikuwa na maombi kadhaa likiwamo ombi hili,“Eee Baba Mungu
sisi ni kama mtoza ushuru, hatuna kitu mbele yako, usikilize sala zetu
katika unyenyekevu tunaokutolea kila siku.”
0 Comments