NA MWANDISHI WETU
SERIKALI
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimeti ya Maafa imeeleza
itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa masuala ya maafa nchini
ili kuendelea kusimamia na kuratibu masuala hayo kwa lengo la kupunguza
madhara yatokanano na maafa.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Afya Moja wakifuatilia mkutano huo.
Akiwasilisha
hotuba kwa niaba ya mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa wakati
wa mkutano wa wadau wa masuala ya Afya Moja uliofanyika katika Ukumbi wa
Edema mkoani Morogoro, Bi.Valentina Sanga alisema lengo la Serikali ni
kuhakikisha masuala ya maafa yanaratibiwa na kusimamiwa kwa ufanisi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mratibu
wa Afya Moja,Bi.Valentina Sanga akiwasilisha hotuba kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Afya Moja walipokutana
mkoani Morogoro kwa lengo la kujadili maendeleo ya Utekelezaji wa
shughuli za Afya Moja.
Mkutano
huo ulihusisha wawakilishi kutoka katika wizara mbalimbali za kisekta,
Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo,
wawakilishi kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma ikiwemo;TAWIRI na
TANAPA, na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR, Waratibu wa
Dawati la Afya Moja pamoja na washiriki kutoka Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
Mshauri Elekezi kutoka Shirikika la Afya Duniani (WHO), Bi.Peragia Muchuruza akiwasilisha taarifa wakati wa mkutano huo.
Alieleza
kuwa, kutokana na matukio ya hivi karibuni ya milipuko ya magonjwa kama
vile janga la UVIKO – 19 ambalo limeathiri nchi mbalimbali duniani;
yamedhihirisha umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika kupambana nayo.
Serikali
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na inaendelea kuimarisha
mashirikiano ya Kikanda na Kimataifa ikiwemo katika eneo la kupambana na
changamoto za majanga yanayovuka mipaka na kuathiri sekta nyingi za
kiuchumi na kijamii.
Afisa
Ufuatialiaji wa Mwenendo wa Maradhi kutoka Zanzibar Epidemiology
Disease Surveillance Unit (ZEDSU) akichangai hoja wakati wa mkutano
huo,kulia ni Mratibu Miradi kutoka Taasisi ya PBA, Bi. Agnes Mushi
akifuatilia.
“Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
itaendelea kuimarisha ushirikiano huu katika eneo la uratibu na
usimamizi wa maafa na magonjwa ya milipuko ikiwa ni pamoja na hatari
nyingine za afya kama Usugu wa vimelea vya magonjwa kwa kuzingatia dhana
ya Afya Moja,”alisema Valetina.
Daktari
Mkuu kutoka Idara Maendeleo ya Mifugo Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji,
Maliasili na Mifugo Zanzibar, Ali Zahran akichangia jambo wakati wa
mkutano huo.
Akieleza
kuhusu dhana ya Dhana ya Afya Moja Valentina alisema ni nyenzo muhimu
ya kiutendaji inayozingatia ushirikiano katika kuandaa na kutekeleza
mikakati ya pamoja ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yanayoathiri afya ya
binadamu, wanyama na mimea ili kutumia kwa ufanisi rasilimali chache
zilizopo.
“Hatua
hii ni muhimu katika kupambana na ongezeko la vimelea vya magonjwa ya
kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda binadamu. Hali ambayo kwa kiasi
kikubwa inachangiwa na mabadiliko ya tabianchi na athari katika
mazingira zinazosababishwa na shughuli za kibinadamu zinazotekelezwa
bila kuzingatia uhifadhi wa bionuai ikiwa ni pamoja na kilimo, ongezeko
la watu, ukuaji wa miji na uvamizi wa binadamu katika makazi ya
wanyamapori,”alisisitizaValetina.
Mhadhiri
kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kutoka Shule
ya Afya ya Jamii, Bi. Gladys Mahiti akifafanua jambo katika Mkutano huo.
Wakichangia
hoja kwa wakati tofauti wajumbe kutoka Wizara ya Afya na Wizara ya
Mifugo na Uvuvi waliahidi kuendelea kutoa ushirikiano pale
unapohitajika na kuendelea kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa ili
kuhakikisha masuala haya yanatekelezwa kwa ufasini na mikakati ya pamoja
katika kudhibiti magonjwa upande wa binadamu na wanyama kwa faida ya
wananchi wote.
Mtaalam
wa masuala ya Afya Moja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dkt.Justine
Assenga akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa masuala ya Afya Moja
katika eneo la mifugo wakati wa mkutano huo.
Naye
Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula Duniani FAO, Dkt. Elibariki
Mwakapeje alisema wataendelea kushirikiana na Serikali ili kuyafikia
malengo yaliyopo.
Washiriki
wa Mkutano wa Wadau wa Afya Moja wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kufunguliwa kwa mkutano wao wa siku mbili Mkoani
Morogoro.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
"Mkutano
huu ni muhimu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kutekeleza masuala ya Afya
Moja, FAO tunatekeleza Sustainable development goals ambapo
tunahakikisha hatuachi nyuma kundi lolote ikiwemo wenye ulemavu, hivyo
tunaamini tutaendelea kutekeleza kupitia mfumo wa Four betters ikiwemo;
better environment, better production, better nutrition and better life
ili kuwa jamii salama," alisisitiza Dkt. Mwakapeje.
0 Comments