NA TITO MSELEM
WIZARA
ya Madini imepokea ugeni kutoka Jamhuri ya Burundi ikiwa ni matokeo ya
kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi
katika Sekta ya Madini.
Kufuatia
kusainiwa kwa makubaliano hayo, ujumbe kutoka Burundi umekuja nchini
Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza namna bora ya
kusimamia rasilimali madini.
Mada
zilizowasilishwa ni pamoja na jiolojia ya Tanzania na jiolojia ya
Burundi, uhusiano wa jiolojia ya Tanzania na jiolojia ya Burundi na
majukumu ya wizara katika kusimamia Sekta ya Madini.
Aidha, ujumbe huo umefahamishwa kuhusu masuala ya uongezaji thamani madini, ushirikishwaji wa wazawa katika uchumi wa madini.
Pia,
ujumbe huo, umepatiwa elimu kuhusiana na maandalizi ya Kufunga Migodi
(Mining Closure), upatikanaji wa leseni pamoja na aina za leseni
zinazotolewa nchini Tanzania.
Akiwasilisha
mada Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga amewataka washiriki
kujifunza kwa weledi mbinu bora za usimamizi wa Sekta ya Madini na
kuuliza maswali yatakayo wasaidia kuboresha usimamizi wa sekta hiyo
nchini kwao.
Ujumbe
kutoka Jamhuri ya Burundi umeongozwa na Mshauri wa Rais katika Sekta ya
Madini wa Burundi Alphonsia Kwizera ambao wamepata fursa ya kutembelea
migodi mbalimbali ya wachimbaji wadogo mkoani Dodoma pamoja na mgodi wa
kati wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Shanta Singida.
Tanzania
na Burundi zilisaini makubaliano ya ushirikiano katika usimamizi wa
rasilimali madini baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Hassan kufanya ziara nchini Burundi ambapo utekelezaji wake umeanza
kufanyika kwa lengo la kuzinufaisha nchi hizo.
0 Comments