NA MWANDISHI WETU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya
ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la
Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock
(SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.
“Kati
ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36
yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki
yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu
na yatatoa huduma zote muhimu.”
Mheshimiwa
Majaliwa ameyasema hayo leo Oktoba 24, 2022 mara baada ya kutembelea
kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea
Kusini.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje
kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo
mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli.
“Mnakiwanda
kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam
kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha
sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa
kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu
kama hiki Tanzania.”
0 Comments