NA MWANDISHI WETU
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na
Uratibu, Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa jamii kuwekeza Dodoma
kwa kuzingatia fursa zilizopo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
za kuendeleza jiji hilo.

Ametoa
kauli hiyo Oktoba 24, 2022 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria ilipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa
Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Akieleza
majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Simbachawene amesema ofisi
yake ina jukumu la kuratibu na kusimamia mradi wa ujenzi wa majengo ya
wizara na taasisi zake, hivyo atahakikisha ujenzi huo unasimamiwa kwa
weledi na kukamilika kwa wakati.

“Hadi
sasa ujenzi umefika asilimia 50 hadi 80 kwa baadhi ya majengo na kwa
upande wa miundombinu ya barabara, nishati, maji na mawassiliano ipo
vizuri hivyo nitoe rai kwa wananchi kutumia fursa zilizopo ili kuwekeza
Dodoma,"amesema Waziri Simbachawene.
Ameongezea kuwa, uwepo wa mji wa Serikali itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa wepesi zaidi.

"Mji
huu ndiyo utafanikisha na kurahisisha shughuli za Serikali kwa urahisi
kwani kila wizara itakuwa hapa na itafikika kwa wepesi, na niwakaribiahe
wananchi kuja kupata huduma mahali hapa,"amesema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Joseph Mhagama aliipongeza
Serikali ya Awamu wa Sita kwa namna inavyowezesha ujenzi wa Mji wa
Serikali kwenda kwa kasi na hii inafaa kuungwa mkono.

"Ninampongeza
Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza
Mji huu, na Kamati imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi hivyo
ninawapongeza ofisi ya Waziri Mkuu kwa kufanya kazi kwa weledi,”amesema
Dkt. Mhagama.
Akitoa
neno mjumbe wa kamati hiyo Mhe.Asha Abdallah ametoa kongole kwa kazi
kubwa inayofanywa na serikali huku akiwaasa watanzania kutumia mji huo
katika kupata huduma kwakuwa unafikika kwa wepesi.

"Ofisi
hizi kupatikana mahali pamoja ni jambo nyeti litakalopunguza kero kubwa
za wananchi kwani wizara zote zitafikika kwa wepesi, jueni kuwa
serikali haijawatupa inajali sana,"amesema.
Naye
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Salum Shafi amesema kila mmoja aone umuhimu
wa kulinda na kutunza majengo yatakayotumika na kuhakikisha wanakuwa
wazalendo.

"Mradi
huu ni fedha za walipa kodi, hivyo kila mmoja awe mzalendo katika
kutunza na kulinda yaweze kutumika kwa muda mrefu katika ubora wake na
kuongeza tija katika shughuli za Serikali ,hakika Dodoma imepambika na
mama ameifanya kazi vizuri mama tunakupongeza,”alisisitiza.
0 Comments