Ticker

6/recent/ticker-posts

NIT KUPOKEA ITHIBATI MBILI ZA MAFUNZO KOZI YA UHANDISI WA MATENGENEZO YA NDEGE NA UENDESHAJI


CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimepokea ithibati mbili za mafunzo ya kozi ya usafiri wa anga yaani kozi ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege na uendeshaji wa safari za ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

TCAA ilikabidhi ithibati hiyo mwisho mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Allon Kisaka.

Kisaka alisema kupatikana kwa ithibati hizi kutoka TCAA ni hatua kubwa sana kwa Taifa hasa katika kipindi hiki wakati serikali inaendelea kuimarisha kampuni ya ndege ya Tanzania na sekta ya usafiri wa anga kwa ujumla.

Alisema matunda ya NIT ya kuweka nguvu kubwa katika sekta ya usafiri wa anga yameonekana kwenye ithibati mbili walizozipokea ambapo ni ishara ya chuo kuhakikisha kimetimiza malengo yake na kutoa mafunzo ya kiwango cha Kimataifa.

Alisema ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa kwa haraka serikali imekuwa ikiongeza bajeti mwaka hadi mwaka, ambapo huo ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati ya Serikali kuunga mkono sekta hiyo ambayo ndiyo kiungo muhimu kwenye uchumi.

"Na kwa mwaka huu wa fedha 2020/2023 ATCL inatarajia kupata ndege zingine nne ambazo tayari mikataba yake ilishasainiwa na inaendelea kutekelezwa na hivyo kuanzia Januari, Machi mwakani tutaweza kuona ndege zingine zikiingia,"alisema

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, TCAA, Teophory Mbilinyi alisema amesoma takwimu za usafiri wa anga katika miaka 20 ijayo zitanunuliwa ndege mpya milioni 25 ambazo zinaingia kwenye biashara.

Pia, kwa sasa kuna upungufu wa tekinishani 480,000 duniani, lakini pia wanasema Marekani asilimia 73 ya wataalam wa sekta hiyo wanaenda kustaafu kufikia mwaka 2024.

"Kutokana na kuwepo na gepu hilo duniani, uwezo wa hiki chuo na mafunzo mnayoyatoa ni mwafaka kwa kwa namna ambavyo dunia inakwenda tuna kuwa na upungufu wa watalaamu wa anga wakiwemo mapairoti,"alisema

Naye, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mganilwa alisema wanaomba kipindi bajeti inatengenezwa Serikali iangalie katika maeneo mawili ya uchumi wa bluu, huwa hawahitaji fedha nyingi kwa sababu wao sio kama ATCL ambao wao wananunua ndege.

"Sisi tunahitaji sh bilioni tano, sita kwa mwaka mkitupa kwa miaka minne mtaona miujiza kwa sababu tutakuwa tumeweka miundombinu, tukiajili kijana katika chuo hiki na wenyewe watafurahi,"

"Kwa hiyo suala la rasilimali watu katika sekta ya usafirishaji ikibidi muongeze kidogo fedha kidogo ili chuo kiweza kutekeleza majukumu yake vizuri,"alisema

Alisema kama TCAA walivyowapatia ithibati ya uhudumu wa ndani ndege hawakuwahi kuwaangusha, kwa hiyo anaahidi ithibati walizozipata watazalisha wataalam stahiki ili malengo yaliyokuwa katika usafiri wa ndge yaweze kutimia.

"Na hizi ithibati mbili kitakachokwenda kutokea katika miaka mitano au 10 ijayo tutaanza kuona wawekezaji wazawa wakija kuwekeza kutokana na hatua tuliyofikia kwa sasa,"alisema Profesa Mganilwa

Post a Comment

0 Comments