Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akizungumza katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
************************
Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu amesema Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Ameyasema hayo katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kamati hiyo inashirikisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Umma na binafsi ambao wanahusika na utekelezaji mpango huo.
Amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuifungua Tanzania kwa kuhakikisha inavutia mitaji ya ndani na nje ya nchi kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.
Aidha, Bw. Gugu amesema MKUMBI unalenga kuchochea juhudi ambazo Serikali imeshaanza kuzifanya katika kuboresha mazingira ya biashara nchini, mathalani “Kupitia MKUMBI Serikali imefanikiwa kuondoa tozo takribani 232 zilizokuwa zinafifisha ufanyaji biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo”.
Naye Mkuu wa Msafara wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Africa Mashariki , Bw. Cedric Merel amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa MKUMBI ni makubwa na yanatia moyo na matokeo yameanza kupatikana hususani katika awamu ya nne ya ufanyaji wa biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.
“Mpango huo utatangazwa February 23-24/2023, Tanzania itakuwa katika nafasi nzuri ya kuonyesha mafanikio makubwa jinsi inavyovutia wawekezaji nchini. Hili ni jambo muhimu katika kuvutia wawekezaji wapya kuona maendeleo ya uchumi wa Tanzania na kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka Ulaya kuwekeza hapa.
Naye Meneja mradi wa Ufunguo, Joseph Manirakiza akizungumza kwa niaba ya UNDP alisema wamejikita zaidi katika kusaidia makampuni changa kwa kuwa zitasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Mradi wa MKUMBI unatekelezwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na UNIDO na UNDP kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Msafara wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Africa Mashariki , Bw. Cedric Merel akizungumza katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Msafara wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Africa Mashariki , Bw. Cedric Merel akizungumza katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam.Wadau wa Kamati wakiwa katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Wadau wa Kamati wakiwa katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akiwa na Mkuu wa Msafara wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Africa Mashariki , Bw. Cedric Merel wakipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika kikao cha Kamati Uongozi ya Mradi wa Business Environment, Innovation and Growth (BEGIN) unaofadhili baadhi ya shughuli zilizoanishwa kwenye mpango kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI). Kikao hicho kimefanyika Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments