Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akiwa pamoja na wadau wa NIC wakizindua huduma mpya ya Bima ya BeamLife iliyofanyika Desemba 22,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akiwa pamoja na wadau wa NIC wakizindua huduma mpya ya Bima ya BeamLife iliyofanyika Desemba 22,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Bima za Maisha (NIC) Bw.Hardbet Polepole akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.Watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakipata picha ya pamoja katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya BeamLife iliyofanyika Desemba 23,2022 katika Ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limezindua huduma yake mpya ya BeamLife yenye lengo la kuwawezesha watanzania katika kujiweka akiba ili kukua kiuchumi kwa mtanzania mmoja mmoja endapo atakata Bima hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Bw.Lihami Masoli amesema katika mkakati waaliopanga wa kuhakikisha wanaweza kuwahudumia wateja kwa kiwangokikubwa na kuweza kupata faida nzuri wameweza kufanikiwa kutengeneza faida ghafi ya shillingi bilioni 63 kwa mwaka huu kupitia Huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika Hilo.
Amesema watanzania asilimia 0.3 ndio wenye bima ya maisha, hii inadhihirisha wazi uwepo wa soko kubwa la wateja wa huduma za bima ambao bado hawajafikiwa.
"Kwetu sisi NIC Insurance takwimu hizi ni ishara ya fursa kubwa ambayotunatakiwa kufikia kwa ubunifu wa bidhaa na utoaji wa huduma bora". Amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bima za Maisha (NIC) Bw.Hardbet Polepole amesema Bima ya BeamLife imelenga watanzania wote wenye kipato cha juu, cha kati na cha chini
0 Comments