Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KIGAHE ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NCHINI 


Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa wenye wenye lengo la kujadiliana na kushauriana kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya biashara na changamoto zake katika mkoa huo.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (hayupo pichani),wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa wenye wenye lengo la kujadiliana na kushauriana kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya biashara na changamoto zake katika mkoa huo.


Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa wenye wenye lengo la kujadiliana na kushauriana kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya biashara na changamoto zake katika mkoa huo.

..................................

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha wanakuwa Walezi wa Jumuiya za Wafanyabiashara na kuwa nao karibu katika kila jambo wanalotaka kulifanya ili watoe ushauru wenye tija katika kujenga na kustawisha biashara hapa nchini.

Aidha, amewashauri Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Mameya wote nchini kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania kutengeneza mfumo mzuri utakaomfanya kila mfanyabiashara anapotaka leseni ya biashara aipate kwa haraka bila usumbufu.

Kigahe ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa kwa lengo la kujadiliana na kushauriana kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya biashara na changamoto zake katika mkoa…

Post a Comment

0 Comments