Ticker

6/recent/ticker-posts

PUMA YASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA WA MAFUTA NA GESI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Fatma Abdallah (wa pili kuhoto) akimkabidhi mtungi wa gesi kwa mama aliyejiajiri kwa kutumia usafiri wa Bajaji kueendesha maisha yake. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 8,2023 katika kituo cha mafuta cha PUMA kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Fatma Abdallah akisikiliza moja ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na waandishi hao katika tukio hilo.

Meneja Masoko wa PUMA ukanda wa Dar es Salaam na Pwani Andrea Laizer (wa pili kulia) akikabidhi mtungi wa gesi kwa Bernadetha Kimenya mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kujaza mafuta kwenye Bajaji yake, katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Vennessy Chilambo Meneja Masoko na mauzo ya rejareja Kampuni ya PUMA.

Meneja Masoko wa PUMA ukanda wa Dar es Salaam na Pwani Andrea Laizer (katikati) akiwa na Meneja Masoko na mauzo ya rejareja Kampuni ya PUMA Vennessy Chilambo (kulia) wakifurahia jambo na mwana mama aliyepata zawadi ya mafuta na mtungi wa gesi katika hafla hiyo.

Na:Mwandishi Wetu.

KAMPUNI namba moja ya Mafuta ya Puma imeungana na Wanawake wote nchini katika kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kila Machi 8 ya kila mwaka kwa kutoa zawadi Mafuta pamoja na mtungi wa gesi wa kilo sita kwa wanawake wenye ulemavu wanaojihusisha na utoaji huduma ya kusafirisha wananchi kwa kutumia usafiri wa Bajaji.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi ya mafuta na mitungi ya gesi kwa wanawake hao waambanaji , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Fatma Abdallah amesema katika kuadhimisha Siku hiyo Kampuni yao inaungana na wanawake wote katika kusherehekea na wao wameamua kukutana na wanawake wapambanaji katika Jiji la Dar es Salaam.

Amesema Kampuni ya Puma inatambua mchango wa mwanamke katika harakati za kuleta maendeleo lakini wamerijika zaidi kuungana na wanawake wapambanaji hao amba mbali ya kupewa zawadi ya mafuta wamepata na mitungi hiyo ya gesi kurahisisha katika mambo ya mapishi kwenye familia zao.

"Kampuni ya Mafuta ya Puma tunajihusisha na biashara ya Mafuta , vilainishi pamoja na nishati safi ya gesi ya kupikia kwa kuwa na bidhaa ya Puma Gas, kwa siku ya leo tumeamua kutoa zawadi ya kuwajazia mafuta na kuwazawadia mitingi ya gesi wanawake wenye ulemavu ambao wanatoa huduma ya kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam,tunataka wanapofanya shughuli zao wasifikirie kuhusu kutumia Kuni na mkaa wanapotaka kupika.

"Lakini kutoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa wanawake hawa wenye ulemavu ,gesi hii ambayo tumeitoa kama zawadi kwa wanawake hawa wapambanaji pia ni sehemu ya kampuni yetu kuuungana mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mstari wa mbele kuhamasisha nishati safi ya kupikia na kuachana na Kuni na mkaa, hivyo pamoja na mambo mengine tunatumia sku hii ya Wanwake duniani kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia"

Kwa upande wake Safia Abdallah ambaye ni mmoja wa wanufaika wa majiko na mafuta yaliyotolewa na Puma, ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuwakumbuka katika kuadhimu siku ya Wanawake Duniani na kwamba wao ni wapambanaji hivyo wataendelea kupambana huku akisisitiza kauli mbiu ya Rais Samia Suluhu Hassan inasema kazi iendelee,hivyo wanaendelea kuchapa kazi.

Machi nane kila mwaka, wanawake huadhikisha siku ya wanawake duniani kwa lengo la kuwakutanisha kwa pamoja ili kujadili fursa na changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.


Post a Comment

0 Comments