Ticker

6/recent/ticker-posts

MFUKO WA ELIMU WA TAIFA WATUMIA MILIONI 750 UJENZI WA SHULE YA MTAALA WA KIINGEREZA JIJINI DODOMA.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Umma ya Mchepuo wa Kiingereza ya Msangalalee Jijini Dodoma Bi Dina Mndesha akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Umma ya Mchepuo wa Kiingereza ya Msangalalee Jijini Dodoma Bi Dina Mndesha( wa kwanza kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Umma ya Mchepuo wa Kiingereza ya Msangalalee Jijini Dodoma Bi Dina Mndesha( wa pili kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shule hiyo
Wanafunzi wa darasa la awali wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza Msangalalee wakiwa Darasani.
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingeeza ya Msangalalee , Bw. Masumbuko Paulo akifundisha darasani.
Jengo la Madarasa la Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Msangalalee

********************

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa inaousimamia imetumia Sh. Milioni 750 kufadhili ujenzi wa Shule ya Msingi Msangalalee ya mtaala wa Kiingereza ambayo imeanza rasmi muhula wa masomo Januari 2023 kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari waliotembelea shule hiyo leo tarehe 18 Aprili, 2023, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi Dina Mndesha amesema shule hiyo ya umma kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 215 ikiwa na walimu 16.

‘Naishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu kwani shule hii ya mchepuo wa kiingereza imekuwa shule ya umma ya mfano kutokana na ubora wa miundombinu yake katika jiji la Dodoma, amesema Mndesha Mwalimu Mkuu wa shule hiyo”

Ameongeza kuwa kumekuwa na idadi kubwa ya maombi ya udahili na kwamba wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo wanatoka sehemu mbali mbali za jiji la Dodoma.

Kuhusu mikakati ya kuhakikisha shule hiyo inafanya vizuri, Mwalimu Mndesha amesema, wamejiwekea utaratibu wa kuwatambua na kuwapa motisha walimu ambao wanafunzi wao wanafanya vizuri katika mitihani ya kila mwezi.

Aidha, uongozi wa shule unafanya kazi kwa karibu na wazazi wa wanafunzi ili kuhakikisha wanafunzi wanazingatia masomo, pale tunapoona mwanafunzi analega katika masomo tunawasiliana na mzazi ili kupata suluhu.

Mfuko wa Elimu wa Taifa umetoa ufadhili wa Sh. milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo itakayotoa elimu kwa lugha ya kiingereza katika mwaka wa fedha wa 2021/ 2022 kwa lengo la kusaidia jitihada za Serikali za kutoa elimu bora.

Ujenzi huo umejumuisha jengo la utawala, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.





Post a Comment

0 Comments