Ticker

6/recent/ticker-posts

ROYAL TOUR NI ZAIDI YA FILAMU – DKT. ABBASI

Na John Mapepele

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi amesema mwaka mmoja baada ya kutengenezwa kwa Filamu ya tisa duniani ya Royal Tour nchini Tanzania iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Samaia Suluhu Hassan kumekuwa na mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii ambapo amewataka watanzania kutumia kikamilifu fursa mbalimbali zilizoletwa na Royal Tour kujiongezea vipato vyao na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Dkt. Abbasi ameyasema haya leo, Aprili 28, 2023 kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Royal Tour kwenye kumbukizi la mwaka mmoja ya Filamu hiyo huku akimpongeza Mhe. Rais Samia kwa maono yake ya kuamua kuicheza filamu hiyo ambayo imeifungua Tanzania duniani katika Nyanja mbalimbali na pia kuwa filamu ya Royal Tour inayoongoza kukubalika kuliko zote zilizowahi kufanyika hapa duniani.

Ameyataja baadhi ya mafanikio ya Filamu hiyo yaliyopatikana katika kipindi hiki cha mwaka mmoja kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa watalii nchini ambapo mapato ya jumla ya sekta hii yameongezeka kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na TZS Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani 2,527.77 (sawa la TZS Trilioni 5.82) ambapo amesema kwa upande wa taasisi za Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa) na Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) pia zimevunja rekodi ya mapato.


“Tanapa kwa miezi tisa tu (Julai, 2022-April, 2022) imevunja rekodi kwa kupata jumla ya watalii 1,412,719, idadi ambayo hawajawahi kuipata tangu ianzishwe; wakati NCAA kwa miezi tisa tu kama Tanapa tayari wana watalii 638,950 na mapato ya TZS Bilioni 146.33 ambayo hawajawahi kuyapata. Watalii wanaotembelea maeneo ya misitu (TFS) na uwindaji na picha (TAWA) wameongezeka kutoka 96,150 hadi 218 na 38,000 hadi 159,000 mtawalia kati ya mwaka 2021 na 2022.” Amefafanua, Dkt. Abbasi.

Aidha amesema hamasa ya Royal Tour pia imeongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ambapo amesema kuwa watalii kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 620,867 mwaka 2020 hadi 1,454, 920 Disemba, 2022 sawa na ongezeka la asilimia 57.7 na kufafanua zaidi kuwa kwa takwimu za mpaka Machi, 2023 Tanzania itavunja rekodi ya Taifa kwa watalii kutoka nje; ambapo watalii wa Ndani wameongezeka kutoka 788,933 mwaka 2021 hadi 2,363,260 mwaka 2022.

Akizungumzia kuhusu kuongezeka kwa uwekezaji, Dkt. Abbasi amesema kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha Biashara nchini (TIC) hamasa na mguso wa filamu ya Royal Tour umeongeza idadi ya wawekezaji nchini kwa namna mbili: Mosi uwekezaji wa Jumla ambapo amesema akiwa Marekani wakati wa Royal Tour, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alishuhudia mikataba ya awali 8 (miwili ikihusu sekta binafsi na sita ya kiserikali) ambapo uwekezaji wake ni zaidi ya TZS Trilioni 11.7


Aidha, baadhi ya wawekezaji hao wameshafika nchini na kupewa ardhi kama kampuni ya Camdemi HB (Hotel Arumeru); kampuni ya Polo Properties imeshasajili mradi TIC na kampuni za Northern New Feed zimeshafika nchini na taratibu zinaendelea; Pili amesema filamu imesaidia uwekezaji mahsusi kwenye Sekta ya Utalii ambapo amefafanua kuwa TIC imeshuhudia ongezeko la miradi ya uwekezaji wa kitalii ikiwemo kusajiliwa Mradi Mkubwa wa Dola Milioni 300 uitwao Tourism Adventure Park utakaokuwa na hoteli, maeneo ya utalii wa kiutamaduni na michezo.
Hadi Machi, 2023, jumla ya miradi mikubwa 26 ya uwekezaji katika utalii imesajiliwa, ikilinganishwa na miradi 16 Machi 2020 (kabla ya Royal Tour). Kuhusu mafuriko ya Ndege katika kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).


Dkt. Abbasi amesema hamasa iliyotokana na Royal Tour pia imekuwa na manufaa kwa sekta ya usafiri wa anga na kueleza kuwa ndege za kimataifa zimeongeza ruti nchini na miruko ya jumla ya ndege za kimataifa imeongezeka kwa asilimia 28 kutoka miruko 6,115 Aprili 2021 hadi 7,850 Aprili, 2023;

Akitolea mfano amesema shirika la ndege la Qatar Air na KLM yaongeza miruko kwa Siku ambapo mashirika hayo zameongeza miruko kutoka 9 hadi 12 (ndege mbili kwa siku) na miruko 5 hadi 6 mtawalia pia shirika la ndege la Eurowings Discover (Lufthansa Group) limeanzisha safari zake kuanzia Juni 2022 kuja Tanzani mara mbili kwa wiki moja kwa moja kutoka Frankfurt, Ujerumani kuleta watalii wa Ujerumani na Ulay kwa ujumla.




Post a Comment

0 Comments