Ticker

6/recent/ticker-posts

YALIYOJIRI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA VIPIMO DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOA WA KIGOMA.


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Isack Mwakisu akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amefungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo kitaifa yamefanyika Mkoa wa Kigoma. Kongamano hilo kimehudhuriwa na Viongozi wa Mkoa wa Kigoma na vikundi mbalimbali vya Wakulima wa Mkoa wa Kigoma.

Katika ufunguzi ameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kuadhimisha Siku ya Vipimo Duniani yenye kaulimbiu "Vipimo katika kuwezesha mfumo wa usambazaji wa chakula duniani".

Kadhalika, Kanali Mwakisu ameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kuona umuhimu na kutengeneza seti ya Vipimo 25 vya ujazo wa Lita 5, Lita 10 na Lita 20 ambavyo siku ya leo vitagawiwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na vikundi 24 vya Wakulima na wauzaji wa Mawese Mkoani Kigoma.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa ameeleza kuwa imefika wakati wa sote kwa pamoja kusema matumizi ya Vipimo batili maarufu kama bidoo sasa basi ndio maana Wakala wa Vipimo imeleta seti 25 za Vipimo na kuvigawa kwa makundi mbalimbali ili kuhimiza matumizi sahihi ya Vipimo kwenye uuzaji wa Mawese.

Pia, Bi. Stella ameziomba halmashauri kuona umuhimu wa kuongeza idadi zaidi ya ununuzi wa Vipimo ili kuweza kuwalinda Wakulima na wafanyabiashara kwa kuhakikisha Biashara zinafanyika kwa haki na usawa kwa kila upande bila kupunjana.

IMEANDALIWA NA SEHEMU YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA WAKALA WA VIPIMO

Post a Comment

0 Comments