Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Edward Mpogolo amesema Serikali itaendelea kufichua kampuni zote ambazo zinafanya kazi kinyume na maadili ikiwemo kutosajili kampuni zao.
Ametoa kuali hiyo Jijini Dar es salaam katika warsha ya uhamasishaji wadau kuhusu kanuni za wamiliki manufaa iliyoandaliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni –BRELA na kuwakutanisha chama cha mabenki Nchini.
Amesema mwaka 2020 kupitia sheria ya makampuni serikali imefanya marekebisho mbalimbali ikiwemo kuongeza kipengele cha umiliki manufaa ili kuzifanya kampuni zote ambazo zimesajiliwa hapa nchini kutambulika huku akisema sheria hiyo haijalenga kumkandamiza mwekezaji.
Nae Mkurugenzi wa Leseni Bw. Andrew Mkapa amesema BRELA imeona kuna umuhimu wa kutoa elimu hiyo kwa kuwashirikisha wadau kutoka kwenye sekta ya Benki.
"Hii ni baada ya mabadiliko ya sheria yaliyopitishwa na Bunge la JMT na kupitishwa kwa kanuni za Umiliki Manufaa na Waziri mwenye dhamana ya Biashara imeonekana ni muhimu sana kutoa elimu hii kwa wadau tunaofanya kazi kwa pamoja ". Amesema Bw.Mkapa
Amesema kupitia warsha hiyo itaibua michango mizuri na kuwezesha kuwa na uelewa wa pamojaambao utasaidia kufanikisha zoezi hilokwa manufaa ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi usajili wa makampuni na majina ya biashara –BRELA, Isdor Nkinda amesema uwasilishaji wa taarifa wa umiliki manufaa ni takwa kisheria huku yeyote atayakae toa taarifa za uongo adhabu yake ni kifungo au faini.
Tusekelege Joune ni Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Mabenki nchini amesema chama hicho kitaendelea kushirikiana na serikali katika kuwabaini wale wote ambao sio wazalendo hasa katika uhalifu wa kifedha.
BRELA imewahakikishia wamiliki wa kampuni kuwa itaendelea kutoa elimu kabla ya adhabu hivyo wanapaswa kusajili kampuni zao lengo ni kuondoa migogoro baina ya serikali na wenye kampuni.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Edward Mpogolo akizungumza wakati akifungua warsha ya uhamasishaji wadau kuhusu kanuni za wamiliki manufaa iliyoandaliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni –BRELA na kuwakutanisha chama cha mabenki Nchini. Mkurugenzi wa Leseni Bw. Andrew Mkapa akizungumza katika warsha ya uhamasishaji wadau kuhusu kanuni za wamiliki manufaa iliyoandaliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni –BRELA na kuwakutanisha chama cha mabenki Nchini.
Wadau mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa warsha ya uhamasishaji wadau kuhusu kanuni za wamiliki manufaa iliyoandaliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni –BRELA na kuwakutanisha chama cha mabenki Nchini.
0 Comments