NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesaini hati za Makubaliano kuhusu Mashirikiano katika Ukaguzi na Usajili wa Majengo ya Chakula na Vipodozi na Wakurugenzi Watendaji wa Manispaa zote jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati akifungua hafla ya kusaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya serikali za mitaa mapema leo Juni 20, 2023 jijini Dar es salaam, Kaimu Katibu Tawala , Dar es Salaam Mhandisi Amani Mafuru amesema kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano (MoU) kutaongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wakati bila kuathiri vigezo vya ubora na usalama.
Amesema asilimia 40% ya makusanyo yatokanayo na ukaguzi wa usajili kwa mujibu wa makubaliano, yatakwenda halmashauri.
"Halmashauri mkazitumia fedha hizi katika kutekeleza majukumu hayo na kuendelea kujenga uwezo ikiwa ni pamoja na kuongeza vitendea kazi". Amesema Mhandisi Mafuru.
Aidha ametoa rai kwa Wakurugenzi kutenga sehemu ya mapato yatokanayo na mgawanyo wa asilimia kama ilivyooneshwa kwenye MoU kununua vitendea kazi zaidi.
Pamoja na hayo amewaomba viongozi waliofika kwenye hafla hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa majukumu hayo katika Halmashauri zao
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk.Athuman Ngenya amesema ushirikiano huo na halmashauri utaenda kusaidia afya za wananchi kulindwa kwa kuhakikisha wanatumia bidhaa zilizo bora pamoja na kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk.Athuman Ngenya (kulia) akisaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na Mamlaka ya Serikali za mitaa mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Katibu Tawala (M) Dar es salaam Mhandisi Amani Mafuru akikabidhi vishikwambi kwa watendaji wa Halmashauri za Manispaa ya Mkoa wa DSM, kama kitendea kazi kwa ajili ya shughuli za usajili wa majengo ya chakula na vipodozi wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano na TBS
Kaimu Katibu Tawala (M),Dar es salaam Mhandisi Amani Mafuru akifungua hafla ya kusaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya serikali za mitaa mapema leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya serikali za mitaa mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki Fransis Mapunda akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya serikali za mitaa mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti ubora Dkt.Ashura Katunzi Kilewela akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano(MoU) kati ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na mamlaka ya serikali za mitaa mapema leo jijini Dar es salaam.
0 Comments