Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS: TANZANIA KUIWAKILISHA AFRIKA BARAZA KUU LA UTALII DUNIANI, YANG’ARA PIA UTENDAJI UNWTO

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ataliwakilisha Bara la Afrika katika nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Baraza Kuu (General Assembly) la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).

Tanzania imepitishwa kwa kauli moja jioni ya leo Julai 26, 2023, katika Mkutano wa UNWTO Kanda ya Afrika kuliwakilisha Bara la Afrika na nafasi hiyo ya Tanzania itathibitishwa rasmi kiutaratibu tu (formality) kwenye Mkutano Mkuu wa UNWTO Oktoba mwaka huu mjini Samarkand, nchini Uzbekstan.

Kwa nafasi hiyo Waziri Mchengerwa atakuwa Makamu wa Rais wa Baraza hilo linalofanya maamuzi mengi makubwa duniani kuhusu utalii kwa niaba ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa kipindi cha miaka miwili.

Muda mfupi uliopita tena majira ya saa tatu usiku huu nchini Mauritius Tanzania imeshinda tena nafasi nyingine muhimu katika UNWTO ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu. Kamati hiyo ndiyo huchambua Bajeti na miradi ya kutekelezwa kabla haijapelekwa kwenye Baraza Kuu la UNWTO.

Nchi 13 za Afrika ziligombea nafasi hiyo ya utendaji na zilitakiwa 6, ambapo katika kura zilizopigwa Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi sita zilizopata kura nyingi na sasa, kiutaratibu tu tene, zitaidhinishwa katika Mkutano wa Oktoba, 2023.

Katika hatua nyingine mwishoni mwa Mkutano huo Tanzania imeng’ara tena kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa Wajumbe wa Kikosikazi cha Kuitangaza Afrika (Rebrand Africa Working Group).

Post a Comment

0 Comments