Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 14,2023 jijini Dodoma kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) Prof.Appolinaire Djikeng,akizungumza kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Afisa Programu kutoka AGRA Bw.Donald Mizambwa,akizungumza kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi kutoka Shirika la Dalberg Bw.Jackson Mahenge,akizungumza kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji (Wizara ya Mifugo na Uvuvi) Dkt. Nazael Madalla ,akizungumza kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 14,2023 jijini Dodoma kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imeanza kutekeleza mkakati maalumu wa kukabiliana na tatizo kubwa la kufa kwa mifugo kwa kukosa chakula na maji wakati wa kiangazi kwa kuanzisha mashamba makubwa ya malisho katika halmashauri 44 zinazoathirika mara kwa mara na tatizo hilo.
Hayo yamebainishwa leo Julai 14,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Waziri Ulega amewataka wadau wa Mifugo na uvuvi nchini kuwa na utayari wa kushiriki mkutano huo (AGRF)ili kujadili mikakati na hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa chakula barani Afrika,ustawi wa uchumi na kuwezesha Afrika kuzalisha chakula na kujilisha yenyewe.
"Sisi kama Serikali tulianzisha mkakati wa mashamba darasa Kwa halmashauri 44 zenye Mifugo Kwa kuanzisha mashamba zaidi ya 100 ili kuwaonesha wafugaji kuwa inawezekana kulima,kuvuna na kuhifadhi Kwa faida zaidi,hii itaenda sambamba na urasilimishaji wa Kilimo cha majani na uhifadhi wa ardhi,pomoja na kuwa na Ranchi za asili,"amesema Waziri Ulega
Amesema kuwa Tanzania inaenda kuwa mwenyeji wa mkutano huo hivyo Ushiriki wa wadau wa kisekta watanufaika na fursa zitakazopatikana ikiwemo kukutana na wafanyabiasha mashuhuri na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali hali inayotazamwa kufungua milango ya uwekezaji na mashirikiano kibiashara.
“Tumejipanga kuongeza uzalishaji Kufuatia jitihada za Rais Samia,tumejipanga kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuuza ziada ya mazao ya mifugo na uvuvi katika nchi nyingine “amesema Ulega na kuongeza kuwa
“Ujio wa mkutano huo kwa Tanzania ni fursa adhimu ya wadau wetu kukutana na wafanyabiashara mashuhuri na wawekezaji kutoka katika nchi mbalimbali ulimwenguni ,hivyo itasaidia kufungua milango ya uwekezaji na kuongeza mashirikiano ya kibiashara kwa wadau wetu .”amesema
Aidha amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Mkutano huo September 5-8,2023 Jijini Dar es Salaam.
''Mkutano huo utakaoongwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika pamoja na washiriki zaidi ya 3000 wanaojihusisha na mnyororo wa thamani wa Mifugo na chakula.''amesema Waziri Ulega
Hata hivyo Waziri Ulega amesema kuwa mkutano huo unatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya maonyesho katika eneo la mkutano kwa lengo la kuonesha shughuli zinazofanyika katika minyororo ya mifumo ya chakula nchini lakini pia kutangaza biashara za wadau ili kupata mitaji na masoko ,hivyo ushiriki wa wadau ni muhimu ili waweze kunufaika na fursa hizo.
Pia Waziri Ulega ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wadau kuandaa taarifa za Kampuni zao kwa ufasaha ili iwe rahisi kujitangaza na kuvutia wawekezaji,wafadhili na kuongeza wigo wa biashara zao.
"Nitoe rai kwa wadau ambao maeneo yao yatatembelewa wakati wa AGRF wawe tayari kushiriki kikao kikamilifu katika kutoa taarifa zitakazohitajika Kwa wageni wa AGRF watakao watembelea,kipekee natoa shukrani zangu kwa wenzetu wa ILRI na Dalberg kwa kuwezesha tukio hili,"alisisitiza
0 Comments