Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA CANADA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,akizungumza wakati alipofanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Serikali ya Canada imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufadhili miradi mikubwa katika sekta ya Elimu ikiwamo kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania.

Akizungumza leo Julai 20,2023 Jijini Dodoma wakati wa ziara yake hapa nchini kutembelea miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Canada, Waziri wa Maendeleo Kimataifa na mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan amesema kuwa ameridhishwa na hatua ya utekelezaji na kutangaza kuongeza kiwango cha ufadhili.

Amesema kuwa katika ongezeko la ufadhili watajikita zaidi katika kufadhili miradi wa kila Binti Asome na mradi wa uwezeshwaji kupitia Program za ujuzi utakaogharimu Dola za Canada Milioni 50 ambazo ni zaidi ya Sh.Bilioni 93.

Amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya mradi uitwao kila binti asome utakaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Mradi wa uwezeshaji kupitia programu za ujuzi utakaotekelezwa na Shirika la Vyuo na Taasisi la nchini Canada ambapo kila mradi utagharimu Dola za Canada milioni 25.

“Mradi wa Kila Binti Asome unalenga kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania ili kukuza uwezeshwaji wake na kupata fursa za ajira za staha,”amesema Mhe.Sajjan

Aidha amesema kuwa mradi wa uwezeshaji unalenga kuongeza ushiriki wa kiuchumi kwa wanawake na mabinti wa Tanzania kwa kuimarisha uwezo wa vyuo vya maendeleo 12 na mashirika ya kijamii 16 kutengeneza na kutoa mafunzo ya ujuzi kwa wanawake na mabinti

Amesema mabinti wengi bado wanachangamoto za kujifunza na kukuza ujuzi zinazowakabili mabinti wa Tanzania Bara na Zanzibar kuwa ni pamoja na tofauti za kimuundo, mzigo wa kazi za nyumbani na majukumu ya uangalizi wa familia, ukatili wa kijinsia.

Amebainisha kuwa pia mitazamo na desturi za kimila, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni pale elimu wasichana inapochukuliwa kuwa ya thamani ndogo, hakuna motisha kwao kumaliza masomo kwa kuongeza ni ukweli kwamba shule nyingi hazikidhi mahitaji ya wasichana walio katika kipindi cha balehe.

Ameongeza kuwa "Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake kuwezesha upatikanaji wa elimu, tunawapongeza kwa maendeleo makubwa katika ngazi ya elimu ya msingi ambapo usawa wa kijinsia umefanikiwa, tunampongeza juhudi za kuondoka marufuku ya mabinti wenye ujauzito na mabinti waliojifungua kurejea shuleni," amesema.

Waziri Sajjan amebainisha kuwa kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, Canada imewekeza katika mafunzo madhubuti kwa walimu wa baadaye katika Vyuo 36 vya Ualimu, katika kipindi cha miaka 14 iliyopita, Canada imetoa zaidi ya dola Milioni 250 za kwenye mfumo wa elimu.

Pia amesema italenga kuwezesha mabinti, wenye umri wa miaka ya 10 na 19, kujifunza na kuongeza ujuzi wao ili kuendana na mahitaji ya soko ya sasa na na ya baadaye nchini Tanzania na itatoa fursa za upatikanaji wa njia Bora mbadala za kujifunza kwa mabinti wajawazito na wasichana waliojifungua ambao wemeenguliwa kwenye mifumo rasmi ya elimu.

Kuhusu kutangaza dola za Canada Milioni 25 kwa ajili ya mpango wa Ajira kupitia ujuzi kwa elimu ya Ufundi Stadi, amesema mradi huo unatekelezwa na Shirika la Vyuo na Taasisi za Canada,unalenga kuhamasisha njia mbadala za elimu kwa wanawake na wasichana.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameishukuru Serikali ya Canada kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini inayolenga kwenda kuboresha Sekta ya Elimu.

"Tumekuwa na mahusiano mazuri na nchi ya Canada katika masuala ya elimu, tunataka kuendelea kupeleka watanzania kusoma nchini Canada, wapo wengi wamesoma nchini humo, ishirikiano wetu ni mkubwa na tunauendeleza,"amesema Prof. Mkenda.

Amesema kwa sasa Tanzania ipo katika hatua za mwisho katika kufanya maboresho kwenye Sera na Mitaala ya Elimu katika mabadiliko hayo Serikali imelenga kuimarisha elimu ya ujuzi na ufadhili huu utasaidia sana Serikali kufikia malengo.

Ameongeza kuwa “Sera yetu mwanzo ilikuwa ikitaka elimu ya lazima kuwa miaka 7 kwahiyo watoto wanakawa wanamaliza katika umri wa miaka 13 hadi 14 na walikuwa hawana uwezo wa kujitegemea lakini katika maboresho tunaweka miaka ya lazima 10 na baadaye kutakuwa na mikondo miwili elimu ya kawaida nay a mafunzo ya Amali na ujuo wa ufadhili huu tunaamini tutafanikiwa” amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Taasisi ya Vyuo vya Canada Bi. Denise Amyot amesema program ya Uwezeshaji Kupitia Ujuzi (ESP) inalenga kuimarisha usawa wa kijinsia, inaunganisha Vyuo na Taasisi za Ufundi za Canada na nyingine kutoka nchi Washirika itaendeleza mbinu ya "Elimu Kwa ajira"


Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,akizungumza wakati alipofanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda,akiishukuru Serikali ya Canada kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini inayolenga kwenda kuboresha Sekta ya Elimu mara baada ya Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,kufanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,wakati wa ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Buheti,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,wakati wa ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Taasisi ya Vyuo vya Canada Bi. Denise Amyot,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,wakati wa ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,akimsikiliza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda,wakati alipofanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,(hayupo pichani) akizungumza wakati alipofanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan,akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda,mara baada ya kufanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara hiyo leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.


Waziri wa Maendeleo Kimataifa na Mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada,Mhe. Harjit Sajjan na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya ziara yake kwenye ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 20,2023 jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments