Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKURUGENZI WAKUU, WANUNUZI DAWA NA VIFAA TIBA KUTOKA NCHI 16 ZA SADC WAWEKA MIKAKATI KUBORESHA MFUMO MANUNUZI KUPITIA MSD

Na Said Mwishehe

WAKURUGENZI Wakuu,Watendaji wakuu pamoja na wakuu wa manunuzi wa Taasisi zinazosimamia ununuzi bidhaa za afya kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SDC) wamekutana nchini Tanzania kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu uboreshaji wa manunuzi ya bidhaa za afya katika mfumo wa SADC.

Akizunguza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) nchini Mavere Tukai amesema wakuu hao wamekutana kwa lengo la kuweka mkakati wa ununuzi wa pamoja wa SADC ambao umeanza mwaka 2019 na MSD ndio iliyopewa jukumu la kununua na bado inaendelea.

“Kutokana na changamoto kama vile za COVID-19 pamoja na changamoto nyingine mbalimbali huu uliyumba katikati hapa kwa hiyo Sekretarieti ya SADC na MSD tushirikiane kupitia kuangalia kwanini hatuvuki malengo au hatufiki ambako tumepanga.Pamoja na COVID je kuna kitu gani tunaweza kufanya tukaboresha zaidi , mambo gani tumejifunza SADC kwa muda ambao tumekuwa tukitoa huduma kwa miaka kadhaa.

“Kwa hiyo tulikuwa tumekutana baada ya kazi kubwa iliyokuwa imefanyika na Sekretariet ya SADC na MSD kwa kupata msaada wa Umoja wa Ulaya kuangalia tunafanyaje kuboresha mfumo wa manununuzi wa SADC.Kikao hiki ambacho tumekutana ni kujakupokea taarifa ya mapitio tuliyoyafanya kuangalia maboresho, lakini tunaiwaje MSD kuendelea kuwa mdau mkuu katika ushiriki wote na kwa kuwa bado iko hapa nini kinatakiwa kufanyika kuboresha.

“Sasa timu ile ya wataalam bingwa kushirikiana na sisi tulifanya mapitio, yalikuwepo mapendekezo kadhaa ya muda mfupi, kati na muda mrefu na lengo ni kuhakikisha mfumo huo wa manunuzi kwa nchi za SADC unafanya kazi vizuri , kwa hiyo palikuwa na uwasilishaji wa kilichoonekana kama maeneo ambayo yanafanya vizuri na kwenye changamoto,”amesema Tukai

Hivyo amesema wamekutana kuangalia mapendekezo ya nini kifanyike ili mfumo ufanye vizuri kwani kama inavyofahamika ni mfumo wa manunuzi wa SADC na sio kwamba ni mfumo wa MSD, ni nchi 16 zote zinashirikiana kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa pamoja na wao wamekabidhiwa jukumu hilo kuendesha huo mfumo wa manunuzi kwa nchi hizo

Aidha amesema kabla ya utekelezaji kuna hatua mbalimbali zinafikiwa kwasababu hilo jambo ni la kimataifa sio la Tanzania peke yake , kwa hiyo mapendekezo yote ya timu ya watalaam , wamekuwa na viongozi wa bohari za dawa kutoka nchi 16 na wafamasia wakuu pamoja na viongozi wa Wizara na walichopendekeza wapokee kwenye baraza la SADC makao makuu watakaa kutengeneza taarifa yao kama timu ya watalaam .

“Mapendekezo hayo kama watapitisha tutapewa ruhusa ya kuendelea na utekelezaji , vitu ambavyo vinahusiana na usimamizi wa mfumo mzima, kuna mambo ya rasimali fedha , kuna watu lakini fedha ni muhimu ili mfumo uende vizuri, kuna mambo ya kuboresha mfumo wa kidigitali ili mambo yaende vizuri.Tunafahamu tuko nchi mbalimbali hivyo makaratasi hayawezi kufanya kitu lazima tuwe na mfumo wa kimtandao ambao utatuunganisha, lakini pia kuna vifaa vya kufanyia kazi katika utaratibu wa manunuzi, malipo, mawasiliano utaratibu wa upangaji wa mahitaji vyote hivyo , nani aajiriwe na uwezo gani vyote hivyo tumevizungumza pamoja.

“Na katika kwenda muda mrefu huko mbele tunaangalia hata ikiwezekana huu mfumo wa manunuzi ya SADC isiwe tu kitengo ndani ya MSD , inapokuwa kitengo hata uzito wake na uhuru wake unaminywa, iwe inajitegemea itakuwa hapa Tanzania na MSD inakuwa na uhuru wake.”

Aidha Tukai amesema wakuu hao wameoneshwa bidhaa zinazozalishwa na MSD ikiwemo barakoa ya N-95 lakini wameonesha video za mambo gani yanafanywa na MSD na mabadiliko yanayoendelea katika kubadilisha mifumo, wameenda kwenye ghala na kwenye kiwanda lakini wameuliza maswali mengi maana changamoto ya mifumo inafanana katika nchi nyingi.

“Kwa hiyo kila mmoja anaeleza anapofanya vizuri na anapopata changamoto , kwa hiyo tunashukuru kwa kubadilisha mawazo na uzoefu , kwa mfano kiongozi wetu kutoka Congo alikuwa na mtazamo tofauti, sasa hivi kuna watu wa Moritius ambao nao wanahoji vitu tofauti kwa hiyo mnakuta inasaidia mnapobadilisha mawazo.Tumejifunza .

“Kwa mfano kuna nishati mbadala Zambia wamefanya vizuri sana kwenye maghala yao kwa hiyo na sisi tunatakiwa kuchukua hiyo teknolojia ili kupunguza gharama za uendeshaji lakini wameangalia tunachofanya MSD hatua tulizofika na tunakoelekea wamefurahi na wameridhishwa, kwa hiyo mnapokuta na kuzungumza pamoja na mambo ya manunuzi bado unaona kabisa kuna muelekeo tunaelekea.

Kuhusu mabadiliko yanayoendelea katika ununuzi wa bidhaa za afya , Tukai amesema wako sehemu nzuri kwasababu cha kwanza wanatakiwa kujua wanafanya mabadiliko katika nini , na unafanya mabadiliko kutokana na mahitaji, wamejua changamoto na maeneo yanayofanya vizuri na walifanya tathimini ambayo waliikamilisha mapema namna wanavyofanya kazi na taarifa zinaonesha upatikanaji wa bidhaa za afya kuna mafanikio makubwa, vifaa tiba wameanza kupokea hata vile vifaa changamoto

Awali Mwenyekiti wa wakuu hao kutoka jumuiya ya SADC anayetoka nchi ya DRC Richard Mulamba Biayi amesema amefurahi kuona MSD ambavyo imeendelea kuwa bora kwani uwepo wa dawa za kutosha pamoja na mifumo imara ya kuhakikisha dawa zinafika kwa wadau. “Kupita MSD ukweli tunafurahi sana kwasababu sasa Afrika tunakwenda kuwa moja katika ununuzi wa dawa na vifaa tiba.MSD inatufundisha tusichoke na tusonge mbele.”

Kwa upande wake Elias Katani ambaye Meneja Miradi Msonge kutoka MSD amesema wamekuwa na wakururgenzi kutuoka taasisi za manunuzi za bidhaa afya kutoka SADC na moja ya eneo ambalo wametembelea ni ghala ambalo linatunza miradi misonge na moja ya jambo ambalo wametaka kujua ni namna operesheni nzima kwa maana wanapokeaje bidhaa , wanasambazaje.

“Tumewapotisha na kuwaonesha namna ambavyo tunafanya , wamefurahi kwa kuona ghala lilivyo na namna nzima inavyofanyika na wakawa na maswali mbalimbali mojawapo kujua utunzaji wa bidhaa katika ubaridi, tukawaonesha vyumba vya baridi ambavyo tunahifadhia dawa husika.


“Pia walitaka kujua uwezo wetu wa kutunza , lakini kulingana na viwango vyetu na tukawaeleza tunaruhusu bidhaa zetu kuchina(kuisha muda) chini ya asilimia 0.2 lakini kulingana na sasa kwa ripoti ambazo tunazo kwa miaka miwili tuko chini ya asilimia 0.1 kwa maana ya kwamba tuko nyuma ya kile tulichojiwekea.Lakini tukawaeleza kama nchi jinsi tunavyotoa bidhaa kwenye mfumo wetu wa kawaida.”
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD) Mavere Tukai akizungunza na waandishi wa habari kuhusu mkutano uliokutanisha Wakurugenzi Wakuu pamoja na Wakuu wa Taasisi za Manunuzi ya bidhaa za afya kutoka nchi 16 za Jumuiya ya SADC


Post a Comment

0 Comments