Bodi ya Mfuko wa Barabara, imeendelea kutoa elimu kuhusu majukumu ya Bodi hiyo ikiwemo ya elimu ya matumizi sahihi ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara kwa wananchi wanaotembelea banda la Bodi katika maonesho ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika Kitaifa jijini Mbeya.
Akitoa elimu hiyo Mhandisi Nedrick Godfrey, amewafahamisha wananchi wanaotembelea banda la Bodi hiyo juu ya uwepo wa mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaowawezesha na kuwashirikisha wananchi katika kutoa taarifa za hali ya barabara kupitia simu za kiganjani kwa haraka ili kuwezesha ufanyikaji wa matengenezo ya barabara kwa wakati kupitia Wakala wa Barabara husika.
Ameongeza kuwa uzinduzi wa mfumo huo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara nchini ulifanyika jijini Mwanza,Julai mwaka 2022, na kwamba tayari zaidi ya watu wananchi 15,000 tayari wameingia kwenye mfumo huo na kutoa taarifa au changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wanapotumia barabara katika maeneo mbalimbali nchini.
Sanjari na hayo Mhandisi Nedrick amewaelimisha wananchi juu ya majukumu ya Bodi ya Mfuko wa Barabara ambayo ni pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara, kugawa fedha za matengenezo ya barabara kwa wakala wa barabara nchini pamoja na kufuatilia matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha zinatumika kwa madhumuni yaliyowekwa.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mifumo kutoka Bodi ya Mfuko wa Barababara Jastine Govela, amewaelimisha wananchi na madereva wa vyombo vya moto jijini Mbeya waliopata fursa ya kutembelea banda la Bodi juu ya ushiriki wao katika kuchangia upatikanaji wa fedha za matengenezo ya barabara na namna fedha hiyo inavyotumika kukarabati miundombinu ya barabara nchini.
"Kwa kila lita ya dizeli au petrol inayouzwa kiasi cha shilingi 263 kinakusanywa na kupelekwa kwenye Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya barabara nchini”. Ameeleza Govela.
Imetolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara
Wananchi jijini Mbeya wakipata maelezo juu ya mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaowawezesha kutoa taarifa kwa haraka kupitia simu za kiganjani. Anayetoa maelezo ni Anayetoa maelezo ni Jastine Govela, Mtaalam wa Mifumo kutoka banda la Bodi ya Mfuko wa Barababara kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini humo.
Madereva
wa Bodaboda jijini Mbeya wakipata maelezo jinsi watumiaji wa vyombo vya moto
wanavyochangia shilingi 263 kwa ajili ya matengezo ya barabara kutoka katika
kila lita ya Petroli au Dizeli wanayonunua na namna fedha hiyo inavyotumika
katika kukarabati miundombinu ya barabara nchini. Anayetoa maelezo ni Mhandisi Nedrick Godfrey kutoka katika katika
banda la Bodi ya Mfuko wa Barababara lililopo kwenye viwanja vya John
Mwakangale jijini humo.
Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabara
0 Comments