Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Bw. Geogre Mhina, akizungumza wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi (taftishi) kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma za Majisafi kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Biharamulo (BWUSA) kilichofanyika leo Agosti 31,2023.
Na.Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeendelea kutimiza azma ya Serikali ya Utawala Bora kwa kushirikisha wananchi kwa kukusanya maoni katika mchakato wa kurekebisha bei za huduma za majisafi, kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Biharamulo (BWUSA).
Akizungumza katika Mkutano uliofanyika leo (31.8.2023), Kaimu Katibu Tawala wa Biharamulo, Bw. Pastory Msabila, alisema ushirikishwaji wa wananchi ni kielelezo cha utekelezaji wa kanuni za Utawala Bora katika kuwawezesha wananchi kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wao.
“Nawaombeni tuwe makini, watulivu, tujenge hoja, tushiriki kwa nia njema kabisa, tutoe maoni yetu bila upendeleo wowote, tukiwa na dhamira ya kuhakikisha kuna mizania kati ya watumiaji wa huduma za maji na mamlaka ya maji,” alisistiza.
Wakiwasilisha maoni, wakazi wa Biharamulo waliitaka EWURA, kuhakikisha bei itakayopitishwa, inaendana na huduma
Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Bw. Geogre Mhina aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano huo alisema, mkutano huu ni sehemu ya Taftishi inaofanywa na EWURA kupata maoni ya wadau wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira kabla ya kutoa uamuzi wa kurekebisha bei za huduma za maji ya BWUSA.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Bw. Geogre Mhina, akizungumza wakati wa mkutano huo leo, 31.8.2023.
Baadhi ya wananchi wa Biharamulo wakifuatilia mkutano huo kwa makini.
Wakazi wa Biharamulo wakitoa maoni yake kuhusu marekebisho ya bei za huduma za maji zilizopendekezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Biharamulo.
0 Comments