Ticker

6/recent/ticker-posts

MCHENGERWA AFUNGUA BENKI YA CRDB IKWIRIRI, AWATAKA WANARUFIJI KUCHANGAMKIA FURSA



Na John Mapepele

Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa -CCM kupitia Mkoa wa Pwani na Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefungua Tawi la Benki ya CRDB Ikwiriri huku.

Akisoma hotuba yake wakati wa tukio la ufunguzi wa Benki hiyo Waziri Mchengerwa ameipongeza Benki hiyo kwa kuja na kufungua benki hiyo katika Wilaya ya Rufiji huku akitoa wito kwa wananchi kuchangamkia huduma zinazotolewa na Benki hiyo.

“Ujio wa benki hii ni kitu muhimu sana katika jamii yetu kwa kuwa inakwenda kuwafungua wananchi wetu wa Rufiji kiuchumi kwa kupata huduma mbalimbali za kibenki”. Amesisitiza Waziri Mchengerwa

Amesema Rufiji ni miongoni mwa Wilaya za siku nyingi hapa nchini ambazo zimekuwa na uchumi mkubwa lakini haikuwa na huduma za kibenki ambapo ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta maendeleo makubwa katika kipindi kifupi huku akitoa wito kwa wanarufiji kufanya kazi kwa bidi ikiwa ni namna ya kumuenzi Mhe Rais.

Ameiomba Benki hiyo kuendelea kutoa mafunzo ya biashara kwa wajasiliamali wadogo na wakubwa walio ndani ya Wilaya hiyo ili waweze kufanya biashara kitaalam na kuwekeza mitaji yao kwenye biashara zenye faida.

Kwa upande mwingine amewashauri wananchi wa wilaya ya Rufiji kuwa na tabia ya kuweka akiba katika benki badala ya tabia iliyozoeleka ya kuweka fedha nyumbani.

Aidha ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuwekeza kwenye sekta ya utalii katika wilaya hiyo hatua ambayo amesema itasaidia kupata fedha za kigeni na kutoa mrindikano wa watalii katika sehemu moja ya nchi.

Ametaja baadhi ya maeneo ya kuwekeza kuwa ni pamoja na eneo la kutengeneza zoo za Wanyama pori nyumbani, pia miundombinu ya wageni kama sehemu nzuri za kulala wageni pindi wanapofika nchini.

“Nitoe wito pia kwa wawekezaji kila mkoa kuangalia jinsi ya kutengeneza zoo za Wanyama ili kupanua wigo wa wageni kutembea na kuwaona Wanyama kirahisi katika maeneo ya nyumbani, hii itaongeza mapato”. Amefafanua Waziri Mchengerwa

Post a Comment

0 Comments