Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Anthony Mshandete (katika) pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania Binnaya Srikanta Pradhan (Kulia) wakikata utepe kuashiria mapokezi rasmi ya Betri 64 zenye uwezo wa kuhifadhi nishati jua kwa saa nane kutoka Serikali ya India.
Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan akiongea na wajumbe waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya Betri 64 zenye uwezo wa kuhifadhi nishati jua kwa saa nane zilizotolewa na Serikali ya India kwa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia
Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan (katikati) akiongozana na menejimeti ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia wakielekea katika eneo la kukata utepe katika hafla ya makibhiano ya betri 64.
Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya Betri 64 zenye uwezo wa kuhifadhi nishati jua kwa saa nane kutoka Serikali ya India kwa ajili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia.
Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia wakati wa hafla ya makabidhiano ya Betri 64 zenye uwezo wa kuhifadhi nishati jua kwa saa nane kutoka Serikali ya India kwa ajili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia.
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) imepokea betri 64 zenye uwezo wa kuhifadhi nishati jua kwa saa nane kutoka Ubalozi wa India nchini Tanzania, zitakazowezesha kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) ambayo ina uwezo wa kufanya kazi kwa saa 24.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo leo tarehe 19 Agosti,2023 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Anthony Mshandete alisema kompyuta hiyo inauwezo wa kuchakata data kwa kasi ya hali ya juu na tangu ilipozinduliwa miaka sita iliyopita ilikumbana na changamoto ya nishati pale umeme unapokatika.
Alisema upatikanaji wa Betri hizo utawezesha kompyuta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi kwa manufaa ya taasisi ambapo hutumika kwa ajili ya kufundisha shahada ya pili ya (Master’s Degree) , kuchakata data za Kibailojia pia itatumika kuchakata data kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na itasaidia katika kuhifadhi data nyeti za serikali.
"Kompyuta hii itasidia kuhifadhi data ndani na nje ya Tanzania kwani inauwezo mkubwa katika ufanisi wenye tija katika masuala ya Tehama, na tunashukuru kwa betri hizi ambazo zitawezesha upatikanaji wa uhakika wa umeme katika kufundishia masomo mbalimbali chuoni hapa "Anasema Profesa Mshandete.
Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan alikipongeza kituo cha Umahiri cha Teknolojia Afrika Mashariki, katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kutoa elimu zaidi katika masuala ya TEHAMA (ICT).
Alisema India inatambua mchango mkubwa wa masuala ya teknolojia na kuipongeza taasisi hiyo kwa kutoa elimu katika masuala ya kompyuta.
"India itaendelea kuhakikisha masuala ya Tehama yanakua zaidi na chuo hiki ni sehemu ya kutoa elimu ya Tehama kwani Dunia hii ina mabadiliko mengi katika masuala ya TEHAMA , nawapongeza kwa kuimarisha masuala ya teknolojia " Alisema Balozi Pradhan
Naye Kaimu Mkuu wa Shule ya Masuala ya Tehama, Hesabati na Mawasiliano Dkt, Judih Leo aliishukuru Serikali ya India kwa kuendeleza Ushirikiano na Kituo hicho na kwa kuwezesha upatikanaji betri utakaosaidia Kompyuta hiyo kubwa (Super Computer) inayoyofanya kazi za tafiti kufanya kazi kwa bidii kwani awali walikuwa na changamoto ya umeme pale wanapotaka kufanya kazi zao, lakini sasa uwepo wa betri hizo utawezesha ufanisi zaidi katika utoaji wa mafunzo kwakutumia kompyuta hiyo.
Serikali ya India na Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia imekuwa ikishirikiana kwa karibu katika kuhakikisha teknolojia inakuwa kwa kasi katika kuleta maendeleo kupitia masomo ya TEHAMA.
0 Comments