Mkandarasi wa Kujenga Barabara ya Singida-Kwamtoro-Kebrash-Handeni yenye urefu wa Kilomita 460,Kampuni ya M/s Railways Constructions Engeering amekabidhiwa rasmi barabara hiyo kwa ajili ya kuanza kazi.
..................
Mkandarasi huyo amepokelewa na Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Mhandisi Msama,wawakilishi wa kampuni wakiongozwa na Mhandisi Harold Kitahinda, viongozi wa vijiji vya Makiungu na Mungaa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Unyanghumpi Mussa Mkanga sambamba na katibu wa Mbunge wa Singida Mashariki Ally Rehani.
Mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo ni miezi 66 na mradi una sehemu nne na zitatekelezwa kwa pamoja.
Wananchi walionyesha shangwe na furaha yao ya kuona mradi huo unaanza baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Katibu wa Mbunge Mtaturu Ally Rehani amewapongeza wakandarasi kwa kuja kuanza kazi kama walivyosaini mkataba tarehe 16 June 2023 pale Jijini Dodoma.
"Mh Mtaturu amefurahi sana kwa jitihada hizi za serikali,na amenituma nifikishe salamu zake kwamba yeye binafsi anatarajia kuona mkizingatia muda wa mradi kwani wananchi wameusubiri kwa muda mrefu ili kuboresha huduma za usafiri," amesema.
Kuanza kwa mradi huo kunakamilisha kazi nzuri iliyofanywa na Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ya kupaza sauti bungeni mara kadhaa wakati akiuliza swali na kuchangia mijadala mbalimbali.
0 Comments