Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Watoto wa Shule ya Msingi Maalum ya Buigiri iliyopo Wilayani Chamwino mara baada ya kupiga picha za kumbukumbu kwenye Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika, Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani wakati wakiwa kwenye eneo lenye michoro ya jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan amewasihi viongozi wa dini kulinda maadili kwa vijana na kukemea maovu kwa jamii ili kuendelea kuwa na taifa imara.
Akizungumza Agosti 15, 2023 jijini Dodoma alipokuwa akizindua jengo la kitega uchumi la kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Rais Samia amesema viongozi hao wanapaswa kuendelea kuliombea taifa lidumu katika amani, umoja na mshikamano na kuwafundisha vijana maadili.
Aidha, amesema kwasasa serikali inatekeleza Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora(BBT) unalenga kuwahamasisha vijana kuingia kwenye shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi na kwamba ataangalia namna ya kufanya kazi na taasisi za dini ili kuchagiza mpango huo.
Amelipongeza kanisa kwa kuwajali watu wenye ulemavu na kwamba huo ni utumishi mwema.
Naye, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyikia, Dk.Dickson Chilongani amesema katika jengo hilo kutakuwa na ukumbi ambao utakutanisha vijana wa vyuo na kupatiwa mada za kujadiliana za kijamii, kiuchumi, mila na desturi ili kuwa raia wema na waadilifu.
0 Comments