***********************
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendesha Mafunzo ya Uelewa wa Vipodozi kwa Wafanyabiashara wa vipodozi kwenye Wilaya ya Tabora ambapo wadau wameweza kushiriki na kupatiwa elimu kuhusu majukumu ya TBS katika kudhibiti ubora na usalama wa bidhaa vikiwemo vipodozi vyenye viambata sumu na vilivyoisha muda wa matumizi.
Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Augosti 10,2023 mkoani Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhe. Louis Bura amesema TBS ina majuku ya kuhakikisha bidhaa hafifu zinaondolewa sokoni ili kuwalinda wananchi ambao pengine hawajui madhara yake.
"Tutambue kwamba ni wajibu wa TBS kutoa elimu ya uelewa kwa wafanyabiashara ili wauze bidhaa zinazokidhi ubora na usalama wa Viwango pia wawe na uelewa kuhusu madhara ya matumizi ya bidhaa hafifu". Amesema
Aidha amesema kuwa kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi na mazuri ya kufanya biashara. zikiwemo sera. sheria. kanuni. miongozo na taratibu, wafanyabiashara mna wajibu wa kufanya biashara kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya kati TBS, Bw. Nickonia Mwabuka amesema vipodozi vyenye viambata sumu na ambavyo muda wake umeisha ni hatari kwa afya zetu, ikiwemo ngozi kubadilika na hatimaye kansa ya ngozi, Hii inafanyika hivyo kwa sababu ya uelewa mdogo wa madhara yake katika afya zetu.
"Pale inapotokea wanayabiashara na wananchi kwa ujumla hawana ufahamu wa ubora na usalama wake linalotekelezwa ni wajibu wa TBS kuchukua hatua ya kutoa ufafanuzi wa jambo hili ili wote tufanyekazi kwa mashirikiano na kwa ufanisi". Amesema
0 Comments