MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea na kampeni ya uhamasishaji juu ya Matumizi sahihi ya EFD kwa wafanyabiashara ambapo wametembelea katika Wilaya ya Kinondoni hasa kwa wafanyabiashara na kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya mashine za EFD.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya uhamasishaji juu ya matumizi sahihi ya EFD Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Kinondoni Bi. Husna Nyange amesema kodi sahihi inatokana na kumbukumbu sahihi za kikodi hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo na wanunuzi kudai risiti sahihi za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma. Mabango hayo yamezinduliwa leo Agosti 24, 2023. Kinondoni Dar es Salaam
Kwa upande wake Meneja msaidizi wa huduma kwa mlipakodi Mkoa wa kikodi Kinondoni Bw. Emanuel Lucian Dafay amesema kampeni hii ni endelevu na kwa mkoa wa kikodi kinondoni walianza kwa kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa wafanyabiashara kupitia simu zao za mkoni ili kiwakumbusha juu ya wajibu wao wa kutoa risiti sahihi za efd “wafanyabiashara wa mkoa wetu wa kikodi Kinondoni waliweza kupata meseji za kuwakumbusha umuhimu wa kutoa risiti” alisema.
0 Comments