Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WAVUTIWA KASI SINGIDA MASHARIKI


MDAU wa Maendeleo Sabina Michael amechangia madawati matano yenye thamani ya Shilingi 300,000 katika shule mpya ya msingi ya Mbwanjiki ikiwa ni namna ya kuunga mkono juhudi za serikali na mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu anayehamasisha shughuli za maendeleo.

Akikabidhi madawati hayo ,Sabina amesema kilichomsukuma kuchangia madawati hayo ni furaha ya kujengewa shule kwenye kijiji chao cha Mbwanjiki.

“Madawati haya nimeyatoa kama namna ya kuunga mkono juhudi za mbunge wetu ambaye kwa muda mrefu tumemuona anahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na leo matunda tunayaona, watoto wetu hawatembei mwendo mrefu kufuata shule,”amesema.

Akipokea madawati hayo kwa niaba ya mbunge ,Ally Rehani ambaye ni Katibu wa Mbunge amempongeza mdau huyo kwa kuonyesha uzalendo na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia watoto.

“Maendeleo yanahusisha jamii nzima sio serikali peke yake ama viongozi peke yake,wananchi wenzangu tuige mfano huu mzuri ambao mwenzetu ameuonyesha,”amesema Rehani.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbwanjiki Omari Kulungu akizungumza kwa niaba ya kijiji na uongozi wa shule amemshukuru Sabina kuunga mkono kuchangia madawati hayo ambayo yatasaidia kupunguza tatizo la madawati hapo shuleni.

“Niwaalike wanachi wengine na wadau wenye nia njema,wajitokeze kuendelea kuchangia maendeleo,”amesema.

Post a Comment

0 Comments