Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji(MB) amewataka wakulima hususani wanaozalisha malighafi ya viwanda vya mafuta ya kupikia kuongeza uzalishaji kutokana na uwepo wa viwanda vingi vya mafuta Nchini.
Dkt. Kijaji amebainisha hayo alipotembelea Maonesho hayo ya Wakulima,Wafugaji na Uvuvi yanayofahamika kama Nanenane Kanda ya Mashariki 2023 yanayoendelea kufanyika Mkoani Morogoro.
Waziri Kijaji amesema kuwa Serikali inaagiza zaidi ya asilimia 60 ya mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi hivyo basi wakulima waongeze uzalishaji kutokana uwepo wa viwanda vya mafuta zaidi 771 nchini na hiyo itapelekea Serikali kupunguza uagizaji wa mafuta kutoka nje ya Nchi.
Aidha Dkt. Kijaji amesema kuwa kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Serikali itawafikia wajasiliamali ambao wamekidhi vigezo vya kupata nembo ya utambulisho (tbs) bila malipo yoyote lengo ni kuwasaidia kupata masoko zaidi ndani na nje ya nchi.
Dkt. Kijaji amekuwa Mgeni Rasmi hii Leo ikiwa ni siku ya sita tangu kufunguliwa kwa maonesho hayo Agosti 1, 2023 na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda huku kaulimbiu yake ikiwa ni “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”.
0 Comments