Ticker

6/recent/ticker-posts

CSSC YAVIJENGEA UWEZO VITUO VYA AFYA VYA MAKANISA


Mratibu wa ubora kutoka Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC), Dk David Isaya ,akizungumza wakati wa kikao kikuu cha mwaka cha Tanzania Christian Medical Association (TCMA) kinachoendelea jijini Dodoma.

Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya St Joseph ya Moshi mkoani Kilimanjaro,Dk Sister Hellen Benedict,akizungumza wakati wa kikao kikuu cha mwaka cha Tanzania Christian Medical Association (TCMA) kinachoendelea jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kikuu cha mwaka cha Tanzania Christian Medical Association (TCMA) kinachoendelea jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SHIRIKA la Christian Social Services Commission (CSSC),limeendeleza juhudi zake za kujenga uwezo vituo vya afya vya makanisa ikiwemo namna bora ya jinsi ya kulinda na kukuza mapato na utoaji wa huduma bora katika vituo hivyo. Hayo yameelezwa leo Septemba 5,2023 jijini Dodoma na Mratibu wa ubora kutoka CSSC Dk David Isaya wakati akizungumza kwenye kikao kikuu cha mwaka cha Tanzania Christian Medical Association (TCMA)

Dk David Isaya amesema kazi yao kubwa ni kuwaunganisha pamoja na watoa huduma wengine ili kushirikisha Uzoefu na kuwajengea uwezo watoa huduma Hospitalini

Amesema jukumu hilo wamekuwa wakilifanya tangu kuanza kwa CSSC mwaka 1992 na wamekuwa wakifanya kwa weledi zaidi.

Ameitaja changamoto inayowakabili ni rasilimali fedha na Watu katika sekta ya Afya

Hata hivyo amesema wamechukua hatua kwa kuimarisha mifumo ya uongozi dhabiti na kuzijengea uwezo menejimenti za hospitali pamoja na utoaji wa vitendea kazi.

Amesema wakitoa huduma Bora wataweza kuongeza idadi ya wagonjwa wanaofika katika vituo vyao.

Amezitaja mbinu wanazotumia kuboresha huduma ni kuwa na watu sahihi kwenye vitengo husika na matumizi ya miongozo sahihi katika kutoa huduma za Afya.

Hata hivyo ametoa wito kwa washiriki kuwa makini kufuatilia yale mafunzo ya kuwajengea uwezo pamoja na kuwatafuta pindi watakapokuwa na shida.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya St Joseph ya Moshi mkoani Kilimanjaro,Dk Sister Hellen Benedict, amesema wamejifunza mambo mbalimbali ambayo yanahusika na uwajibikaji na utoaji wa huduma Bora.

Amesema katika kuhakikisha wanatoa huduma bora, Hospitali hizo wamejipanga kuongeza mapato kwa kutoa huduma Bora.

Amesema uwajibikaji unaanza kwa Mkuu wa kituo na wafanyakazi wote kwa kuwa wazi na kujali wagonjwa.

Ni jukumu letu katika mafunzo tuliyopata tunaimarisha maslahi pamoja na yale mahitaji muhimu ya watumishi wetu ili na wao waweze kuwahudumia wagonjwa wanaokuja.

Amesema mgonjwa akipata huduma nzuri ataendelea kuwa mteja pamoja na kuleta wateja wengine kwenye huduma bora.

Kupitia mafunzo haya tumeweza kutoa huduma Bora na tunajivunia huduma zetu na tutaendelea kufanya vizuri zaidi na tunataka kutambulika Kimataifa kama Hospitali Bora inayotoa huduma bora.

Post a Comment

0 Comments