*Wadau wapongeza jitihada za KC Manzese
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Manzese KC Theresia Lihanjala amesema kuwa vitendo vya ukatili katika jamii vinarudisha nyuma ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja aliyefanyiwa ukatili.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa Manzese Theresia amesema kuwa kila mwanajamii kuwa sehemu ya kupinga ukatili katika kutengeneza jamii isiyo na ukatili.
Lihanjala amesema kuwa katika mkutano huo kila mmoja anawajibu wa kutoa taarifa pale panapoonekana kuna ukatili unafanyika kabla ukatili huo hauota mizizi.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mferejini Manzese Sophia Kisuka amesema serikali ya mtaa itakuwa bega kwa beaga na KC katika kupinga masuala ya ukatili.
Afisa Mtendaji amezindua namba 1.5.5 ambapo mtu mmoja akipata taarifa atapeleka kwa watu Watano na hao watano kila mmoja atapeleka taarifa kwa watu watano na hao vile watapeleka taarifa hiyo ili kuwa rahisi kwa ukatili uliofanyika kuchukuliwa hatuo.
Afisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia kituo cha Polisi Urafiki Habiba Kubegeya amesema kuwa kuna vitendo vya ukatili vinafanyika hivyo jamii itoe ushirikiano kwa polisi.
Hata hivyo ameshauri wazazi kuna vitu vya kuiga kwa watoto ambavyo vingo vinafanya kuharibika.
Aidha amesema kuwa KC imefungua milango hivyo kuweka ushirikiano pale panapoonekana mtu kafanyiwa ukatili watu wawe tayari kutoa ushahidi na kufanya kesi kuwa rahisi.
Janeth Mawiza wa Shirika la Wajiki amesema kuwa kukutanisha na jamii ni jambo bora kwani ukatili ndiko unakofanyika.
Amesema masuala ya ukatili lazima kuwa na maarifa katika kufatilia bila ya kuwa na taarifa sahihi yanasumbua na kufanya waliofanya ukatili kubaki kuwa salama.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Manzese (KC) Theresia Luhanjala akizungumza na jamii ya manzese Mferejini kuhusiana na masuala ya Ukatili , jijini Dar es Salaam.
Askari wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Urafiki Habiba Kubegeya akizungumza kuhusiana na masuala ya ukatili na hatua wanazozichukua.
Jamila Kisinga akichangia katika mkutano ulioratibiwa na KC Mabibo.
0 Comments