Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI KWENYE MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa elimu kwa wajasiriamali wadogo na wachimbaji wadogo juu ya umuhimu wa kuwa na bidhaa zilizo thibitishwa na shirika hilo katika Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA mkoani Geita.

Maonesho hayo ambayo yalibeba kauli mbiu isemayo "Matumizi ya Teknolojia Sahihi katika kuinua wachimbaji Wadogo Kiuchumi na Kuhifadhi Mazingira" yamefungwa leo na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah

Akizungumza katika Maonesho hayo leo Sept 30,2023, Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa Bi.Happy Kayeka, amesema wameshiriki katika maonesho hayo kwa sababu ni fursa ya kukutana na wadau mbalimbali na kuwaelezea shughuli zinazofanywa na TBS.

"TBS tumeshiriki maonesho haya kusudi kukutana na wadau mbalimbali, ukiachana na kukutana na wadau wa madini,tumekutana na wadau mbalimbali ambao tumewafikia na kuwapa taratibu za kufuata katika kuandaa bidhaa iliyokidhi viwango"Amesema

Aidha amesema pia kwa wachimbaji wa madini shirika limeandaa Viwango vya madini ambavyo shirika limekwisha viandaa hivyo itakua fursa kwa wachimbaji kukutana na kuleta bidhaa zao TBS.

"Wazalishaji wa bidhaa zingine ambazo hawajasajiliwa itakua fursa kukutana na kuwapa utaratibu,hata hapa tumeona kuna wajasiriamali ambao wana bidhaa za TBS wengine hazina nembo ya TBS hivyo itakuwa fursa kuwapa taratibu zipi kwa kupitia Sido na kuelekea maabara kwa ajili ya kuthibitisha Viwango vya bidhaa zao"Ameeleza Bi.Kayeka.

Post a Comment

0 Comments