NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeshiriki Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa shirika hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha pamoja watumishi katika michezo ili kuboresha afya na kujenga mahusiano mazuri.
Akizungumza hapo jana Septemba 2,2023 katika Bonanza hilo ambalo limefanyika kwenye viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya TBS, Prof.Othuman Chande amewapongeza wanaviwango waliojitokeza kushiriki pamoja na kushangilia katika kipindi chote cha bonanza.
“Hii itasaidia kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kati ya watumishi, kwani utekelezaji mzuri wa majukumu yenu ya kila siku hutegemea sana afya ya mwili na akili”. Amesema
Amesema watumishi na watoa huduma wa Shirika la Viwango Tanzania wameshiriki katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa wavu, kuvuta kamba na michezo ya jadi ambapo mashindano haya yameshindanishwa kiidara.
“Vilevile kupitia michezo hii watumishi hupata burudani na hupunguza msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na kukosa nafasi ya kufanya mazoezi au kushiriki michezo mbalimbali”. Amesema
0 Comments