Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKENDA AONYA WIZI NA UDANGANYIFU MTIHANI DARASA LA SABA


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma kuhusu wizi na udanganyifu wa mtihani ya darasa la saba unaoanza kufanyika kesho nchini.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ameonya wizi na udanganyifu wa mtihani ya darasa la saba unaoanza kufanyika kesho nchini na kuagiza ifanyike kwa kuzingatia kanuni na taratibu.

Akizungumza leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma na waandishi wa habari, Prof.Mkenda, amesema kuagiza wanafunzi wajiepushe na kuandika maneno yasiyofaa kwenye mitihani.

Amewataka Maofisa Elimu na kamati za mitihani kuanzia shule hadi mikoani wafungue macho na kuhakikisha hakuna wizi wa mitihani.

“Tunaendelea kudhibiti wizi wa mitihani kwasababu ya hatua kali ambazo tumeendelea kuzichukua, udanganyifu hasa wizi wa mitihani hasa ule unaoandaliwa na walimu au wenye shule au Maofisa wa serikali unakwaza mfumo wa elimu.”

“Ukimfundisha wizi wa mitihani unamfundisha mtoto wizi mapema sana na inaharibu weledi katika mfumo wetu wa elimu nchini, mwanafunzi atakayepenya kwa wizi wa mitihani madhara katika uchumi wetu yatakuwa makubwa sana,”amesema.

Amesema wizi wa mitihani unafundisha vitendo vya uvunjifu wa maadili.

“Ofisa yeyote wa serikali atakayebainika kujihusisha na udanganyifu wa mitihani tutahakikisha kwamba ana fukuzwa kazi na kushtakiwa, Baraza la mitihani limetoa namba za kutoa taarifa kwa yeyote atakayebaini vitendo hivi apige 0759360000,”amesema.

Post a Comment

0 Comments