Ticker

6/recent/ticker-posts

KATAMBI AITAKA CMA KUSULUHISHA MIGOGORO YA KIKAZI KWA HAKI NA USAWA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekagua bidhaa zinazozalishwa na vijana wanaoshiriki katika maonesho ya wiki ya vijana kitaifa Mkoani Manyara

Na.Mwandishi Wetu, Manyara

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka Watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kutumia haki na usawa pindi wanaposuluhisha na kuamua migogoro ya kikazi inayojitokeza Mahali pa Kazi.

Mhe. Katambi ameyasema hayo Mkoani Manyara alipotembelea banda la CMA ikiwa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Mkoani humo.

Amesema katika kutatua migogoro na kuleta suluhu CMA inatakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni pasipo kuegemea upande ili kuwasaidia wananchi kupata haki zao.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla amesema lengo la CMA ni kumaliza migogoro ya Waajiri na Waajiriwa kwa haki na kutumia muda mfupi katika kuleta suluhu baina yao.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla alipotembelea banda la CMA Mkoani Manyara ikiwa ni wiki ya kwanza ya wiki ya Vijana Kitaifa.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekagua bidhaa zinazozalishwa na vijana wanaoshiriki katika maonesho ya wiki ya vijana kitaifa Mkoani Manyara

Post a Comment

0 Comments