MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki mahafali ya Shule ya Msingi ya Matongo na kuupongeza uongozi wa shule kwa mipango na mikakati waliyonayo katika kusimamia taaluma shuleni hapo.
Akizungumza katika mahali hayo Mtaturu amewapongeza kwa kusimamia taaluma na kupokea Shilingi Milioni 111 za kujenga miundombinu ya shule kwa kipindi cha miaka miwili.
“Hiyo ni dhamira ya wazi ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingirra ya kufundishia na kujifunzia,”.
“Niwapongeze kwa mipango na mikakati yenu mizuri niahidi kuwaletea Mashine ya kurudufu,jiko,gesi na sukari kilo 25,”.ameongeza.
Aidha alitoa zawadi kwa wanafunzi 13 waliofanya vizuri kwenye taaluma,nidhamu na michezo kabla hajakabidhi vyeti kwa wahitimu 156 wa Darasa la saba mwaka 2023.
Kupitia risala ya wanafunzi iliyosomwa na mwanafunzi Bunzali Mbabani ameeleza uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu kwa kuwa walizonazo zimeshakuwa chakavu kutokana na shule hiyo kuwa kongwe tangu mwaka 1947.
“Mheshimiwa mgeni rasmi ili kuboresha taaluma tunauhitaji wa mashine ya kurudufu(photocopy mashine)mitihani ya majaribio kwa wanafunzi kila mwezi na shule inunue rimu za karatasi kupitia fedha za uendeshaji zinazoletwa na serikali,”.amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya ikungihe Abely Nkuwi akitoa salaam kwa niaba ya wananchi na wazazi amempongeza mbunge kwa kuchapa kazi inayoonekana kila mahali.
“Kutokana na juhudi zako kijiji cha Matongo sasa kina shule mpya mbili za msingi Mau na Mbughantiga na Shule mpya ya Sekondari Mosimatongo,nikuombe Mbunge wetu unifikishie shukrani nyingi kwa Rais Samia,”.amesema.
0 Comments