Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,akizungumza wakati akizindua Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
************
Na. WAF, Mbinga- Ruvuma
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini ili kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika
Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati alipo mwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Dkt. Mollel amesema kuwa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi ya Trilioni 6.7 katika sekta ya afya ili kuboresha miundombinu, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendaanishi, kuongeza watumishi wa afya pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa afya kupitia programu ya Samia Scholar ship ndani ya miaka miwili katika sekta ya afya .
“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga nDkt. Sambia amewekeza zaidi ya Bilioni 4 ili kuhakikisha wananchi wa Mbinga wanapata Huduma bora za afya ili kuwa na afya bora na kuendelea na maisha yautafutaji ili kujenga nchini”, ameeleza Dkt. Mollel
Aidha katika kwendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafs Rais Samia amekuwa ni kiunganishi ili kuhakikisha sekta binafsi wanafanya vizuri nchini.
“Leo nipo hapa Litembo katika uzinduzi wa Chuo cha AFYA Litembo hii ni sehemu moja wapo ya serikali kwendelea kuimarisha mashirikiano na sekta binafsi nchini ili kuleta maendeleo kwa Taifa”, ameeleza Dkt. Mollel
Akizungumza amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi imara wa Rais Samia ndani ya mwaka huu imenunua magari ya kubeba wagonjwa 727 na magari 201 yameshafika ndani ya nchini na hivi karibuni yatazinduliwa na kusambazwa katika maeneo yenye uhitaji wa magari ya kubeba wagonjwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo amesema chuo hicho kitakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma na jirani kwani watazalisha wataalamu mbalimbalai wa sekta ya afya na kusaidia kuhudumu katika vituo vya kutolea Huduma za afya nchini.
Amesema kuwa kwa sasa wataanza na kozi ya Utabibu, Wataalamu wa maabara pamoja na wauguzi na chuo hicho kinatarajia kuwa na wanafunzi 360 ambapo kwa sasa wapo wanafunzi 120
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,akizungumza wakati akizindua Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments