Ticker

6/recent/ticker-posts

SBL YAZINDUA PROGRAMU YA SMASHED HUKO TANGA KUDHIBITI KUNYWA POMBE KWA VIJANA WENYE UMRI MDOGO

(26/10/2023, TANGA)— Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited (SBL) inapenda kutangaza muendelezo wa Programu ya Smashed katika Mkoa wa Tanga. Programu hii inatoa ya elimu kupitia maonyesho kwa kulenga kuvunja utamaduni wa kunywa pombe kwa vijana wenye umri mdogo na kupunguza madhara yanayohusiana na pombe kwa vijana. Programu ya Smashed ya Kampuni ya Bia ya Serengeti inawakilisha hatua muhimu kuelekea kukuza uchaguzi wenye dhamira na kuwawezesha vijana wa Tanzania kuwa na maarifa na stadi wanazohitaji kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya pombe na kuzuia kabisa matumizi ya pombe kwa vijana walio chini ya umri wa kisheria.

Utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwaka 2008 miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaam uligundua kuwa asilimia 5 walitumia pombe, asilimia 10.8 walishatumia pombe kabla ya kufikisha miaka 14, na asilimia 26.2 walikuwa na mzazi aliyekuwa anatumia pombe. Matumizi ya pombe wakati wa utoto na ujana yanaweza kuwa na athari mbaya za kiafya, kijamii, kiuchumi, na kimaendeleo kwa vijana na jamii. Utafiti unaonyesha kuwa vijana wanaoanza kunywa pombe kabla ya umri wa miaka 15 wako mara sita zaidi kwa hatari ya kuwa na matatizo ya utegemezi wa pombe kuliko wale wanaoanza kunywa baada ya umri wa miaka 21.

Kutokana na hili, Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited illianzisha programu hii mwaka 2021, na tayari imekuwa na mchango mkubwa kwa vijana wetu. Hadi leo, SBL imefikia shule 22, ikiwaelimisha zaidi ya wanafunzi 24,025 kote nchini. Programu hii haihusishi tu uzuiaji wa kutumia pombe kwa vijana, bali pia kuwezesha akili za vijana wetu kufanya maamuzi yenye msingi na dhamira sahihi. Inawatia moyo wanafunzi kutilia maanani elimu yao na kuendeleza stadi muhimu, kama vile kutawala hisia zao, ambayo itakuwa zana muhimu katika kushughulikia changamoto za maisha.

Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Limited alisema, "SBL inaelewa kuwa shinikizo la rika haswa vijana ni sababu ya kunywa pombe kwa vijana na ni muhimu kukumbuka kuwa una uwezo wa kusema hapana na kufanya maamuzi yanayolingana na thamani ya malengo yako. Marafiki wa kweli wataheshimu maamuzi yako na kusaidia safari yako. Kama wanafunzi, nyote ni sehemu ya jamii kubwa zaidi nje ya shule hizi, na sote tunashiriki jukumu la kujali ustawi wa wenzetu na jamii kwa ujumla. Watie moyo marafiki na wenzako kufanya maamuzi sahihi na kupinga kunywa pombe kwa vijana walio chini ya umri wa kisheria."




Post a Comment

0 Comments