MRATIBU wa Tiba Utalii Dkt.Asha Mahita amesema kuwa kuna umuhimu Tanzania tukajiandaa kwa tiba Utalii na ili iweze kufanikiwa tunahitaji ubora wa huduma kwenye maeneo mbalimbali husika kwa kuzingatia mahitaji maalumu.
Ameyasema hayo jana katika Mkutano wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania imeanza kupokea wageni wengi wanaokuja kufuata matibabu, hii inaonyesha kuwa tayari nchi za Afrika zimeanza kutuamini katika huduma za Afya.
"Ni muhimu sasa hospitali na watoa huduma za Afya waanze kufikiria nje ya box. mwananchi au mgeni apate huduma katika mazingira bora, kwa wakati, yenye utaalamu wa hali ya juu na kuhudumiwa kwa lugha nzuri yenye kumpa matumaini". Amesema
Aidha Dr. Mahita amepongeza jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu akisema kampeni ya Royal Tour imefungua milango kwa watalii wengi kuja nchini, lakini wakati huo.
"Rais amekuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya afya kwani kupitia yeye Tanzania sasa imeanza kupokea sifa katika Tiba Utalii". Amesema Dkt.Mahita.
Naye ,Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Dkt.Caroline Damiani aliwasilisha mada ya Ubora wa Huduma za Afya katika Ngazi ya Msingi wa utoaji huduma za Afya na Muelekeo wa Wizara kuhakikisha huduma bora za Afya zinapatikana nchini
Mkutano wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) ndio mkutano mkubwa zaidi wa kila mwaka wa huduma ya afya nchini Tanzania, unaovutia mamia ya washiriki wa kibinafsi na wa mtandao kutoka kwa mfumo wa huduma ya afya nchini ili kuzingatia maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Mada nyingine zilizotawala.katika Mkutano huo ni kuhusu “Kushughulikia Ukosefu wa Usawa wa Afya ya Mtoto kupitia Ufadhili Endelevu.” Wasilisho lake litachunguza vikwazo nchini Tanzania vinavyozuia upatikanaji sawa wa matibabu ya nimonia ya kuokoa maisha na kuchunguza masuluhisho yanayoweza kusaidia kupanua wigo pia Mkutano huo ulitoa taarifa mpya kuhusu ahadi zilizotolewa na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uwekezaji katika ufadhili wa afya endelevu ambao unapaswa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa Watanzania na kuwezesha nchi kukabiliana na majanga yasiyotarajiwa kama vile janga la Covid-19.
0 Comments