27 Oktoba 2023, Arusha
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) leo, Ijumaa 27 Oktoba 2023 wametoa msaada wa Mashuka 300 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru pamoja na ile ya Jiji la Arusha ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE iliyoanza mapema wiki hii hapa hapa jijini Arusha.
Ujumbe wa TUGHE katika ugawaji wa Mashuka hayo, umeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Cde. Dkt. Jane Madete ambaye ameeleza kuwa TUGHE imekua na utaratibu wa kufanya hivyo mara kwa mara ili kurudisha katika jamii ikiwa na kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali ikiwamo kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Kwa upande wa wawakilishi wa Hospitali hizo wameishukuru TUGHE kwa msaada huo ambao wameeleza kuwa utaenda kusaidia utolewaji wa huduma katika hospital hizo.
Wengine walioshiriki katika tukio hilo ni pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa (KUBK) sambamba na Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wanawake TUGHE Taifa, Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa anayeshughulikia Afya na Oganaizesheni pamoja na viongozi wa Mkoa na wa Matawi ya TUGHE katika hospitali hizo.
IMETOLEWA NA:
Idara ya Habari na Uhusiano
TUGHE
“HUDUMA BORA, MASLAHI ZAIDI”
0 Comments