Ticker

6/recent/ticker-posts

TUGHE YATOA WITO KWA WAFANYAKAZI KUJIUNGA KATIKA CHAMA KIMOJA CHA WAFANYAKAZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimetoa wito kwa wafanyakazi nchini kujiunga katika Chama kimoja cha Wafanyakazi ili kusaidia kuwa na sauti kubwa ya pamoja katika kuhakikisha masuala na stahiki mbalimbali za wafanyakazi zinazingatiwa sehemu za kazi.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Cde. Hery Mkunda alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo.

Katika hotuba yake, Cde. Mkunda amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi katika maeneo ya kazi kujiunga katika Chama kimoja ikiwemo TUGHE ambacho ndiyo kitakuwa chombo cha kuwasemea na kuwasilisha masuala yao mbalimbali kwenye Uongozi na kumrahisishia mwajiri kushughulikia hoja zao kwa wakati kupitia vyama hivyo na pia amewakumbusha wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kufuata taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha Mwajiri anafikia malengo anayokusudia na kwa kufanya hivyo itawaweka katika nafasi nzuri ya kudai maslahi na haki wanayostahili.“Pamoja ya kwamba sheria inaruhusu uwepo wa vyama vingi vidogovidogo, lakini tunapokuwa na Chama kimoja ni sehemu ambayo tunakuwa na sauti kubwa kwa umoja wetu”. Amesema Cde. Mkunda.

Aidha amewasisitizia wafanyakazi kuwa na uwazi hususan katika mambo mbalimbali wanayoyafanya, wawashirikishe viongozi mbalimbali katika mifumo yao ya utendaji waliyonayo sehemu za kazi, wajadiliane kwa pamoja waweze kufikia muafaka katika mambo mbalimbali wanayoyafanya.

Aidha amesema wanaishauri menejimenti kuweza kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha kwamba haki na maslahi ya wafanyakazi sehemu ya kazi vinazingatiwa.

“Tumeona hospitali ya Taifa Muhimbili wanajitahidi, wamehakikisha kwamba wafanyakazi wanapata haki zao kwa muda, na wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa wafanyakazi na kuwapa hamasa wafanyakazi ili waweze kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi”. Ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameipongeza TUGHE kwa kuwa Chama bora kinachosimamia kikamilifu masuala ya Wafanyakazi na kueleza kuwa kila mfanyakazi ana uhuru wa kujumuika mahala pa kazi na pia ni kutimiza takwa la kisheria. Prof. Janabi pia amaongeza kuwa uwepo wa Chama cha TUGHE katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kunamrahisishia sana utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya utendaji wa Hospitali.

Awaliakisoma risala kwa Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuungana nao katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka sambamba na kuelezea mafanikio ambayo wameyafikia na pia ameeleza changamoto walizonazo ikiwemo za kifedha ambazo Mgeni Rasmi pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali wameahidi kuzishughulikia.Nae Katibu wa Chama cha Wafanyakazi tawi la Muhimbili Bi.Tuyeta Elias amesema watayafanyia kazi yale yote ambayo wameelekezwa hasa katika kuhakikisha vyama vya wafanyakazi kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuwa na sauti moja.

Mkutano huo umefanyika kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya TUGHE na umehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Cde. Brendan Maro aliyeambatana na Viongozi wengine kutoka Mkoa huo, baadhi ya Wajumbe wa KUBK, Viongozi wa TUGHE wa matawi ya MOI, JKCI, Muhimbili Mloganzila, Hospitali ya Ocean Road, Amana Rrh, Temeke RRH, Mwananyamala RRH pamoja, watoa mada kutoka OSHA na WCF pamoja na Wanachama wa TUGHE.
Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Cde. Hery Mkunda akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo.

Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Cde. Brendan Maro akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo.
Baadhi ya Wanachama wa TUGHE tawi la Muhimbili wakiwa katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo
.\
Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Cde. Hery Mkunda akipata picha ya pamoja na wanachama wa TUGHE katika Mkutano Mkuu wa TUGHE Tawi la Muhimbili kwa mwaka 2023 ulifanyika leo Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023, katika ukumbi wa CPL,Upanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Wanachama wa TUGHE zaidi ya 400 kutoka tawi hilo.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments