Na Mwandishi Wetu,
MSANII maarufu nchini katika Tasnia ya Filamu za kibongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengele 'Steve Nyerere' amewaomba wasanii wote nchini kuungana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kukomesha matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Aidha amesisitiza watatoa kila aina ya ushirikiano kwa Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kukomesha dawa za kulevya nchini huku akiweka mkakati madhubuti wa kuwalinda wasanii dhidi ya dawa hizo na hatimaye kuwa na wasanii wenye kujikita kulinda vipaji vyao.
Akizungumza Novemba 22, 2023 baada ya kufika ofisi za Mamlaka hiyo na kupokelewa na Kamishina Jenerali Lyimo Stebe Nyerere amewaomba wasanii wenzake wamuunge mkono Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuhakikisha msanii wa Tanzania havuti unga wala havuti bangi.
Amesisitiza ni vema kuona wasanii wakiendelea kufanya sanaa zao kwenye weledi mkubwa ili kusaidia familia zao lakini vile vile kupeperusha bendera ya Tanzania."Kamishina ana nia nzuri sana ya kukuokoa kizazi chetu , Tanzania imebarikiwa na vipaji vikubwa vya kutangaza utamaduni ndani ya nchi na nje ya nchi
"Vipaji hivi kazima tuhakikishe vinaenda na utamaduni lakini vikiwa na hali na afya njema ambayo inapatikana kwa kuwa msaani mwenyewe anajitambua, tunajua wasanii wengi na ni jambo ambalo halifichiki inawezekana bila kupata stimu hawezi kupanda kwenye stegi, bila stimu mtu hawezi kucheza mpira...
" Bila kupata stimu haonekani kama anamuonekano , anataka stimu na stimu zimegawanyika katika hatua mbalimbali , kuna stimu nyingine ya unga, kuna stimu nyingine ya dawa za kulevya na kuna stimu ya Msuba.Lakini kuna stimu hata ya pombe kali lakini hivi vyote vinanyong'onyesha vipaji , hivi vyote vinamharibu msanii wetu kutokuwa na kipaji cha kupeperusha bendera yetu ya dhati, "amesema Steve Nyerere.
Aidha amesema katika mazungumzo yake na Kamishina Jenerali Lyimo amebaini dhamira ya dhati aliyonayo ya kuwapenda wasanii wa Watanzania lakini ameonesha dhahiri yake ya kuhakikisha msanii anafanya sanaa yake katika mazingira yenye afya bora.
" Lakini kikubwa zaidi tunasema yajayo yanafurahisha , ni msanii mwenyewe kujitambua na Kamishina ameelezea hapa jambo jema kwani yeye ni mpenda sanaa na alikuwa anaipenda na enzi zake alikuwa balaa lakini alijilinda mpaka akafika kwenye ndoto yake.
"Kwa hiyo na wasanii lazima tujilinde na tutimize ndoto yetu kwenye sanaa , sanaa ni ajira kama ilivyokuwa ajira nyingine, kwa hiyo ajira yote inalindwa kwa njia yoyote ili ufike malengo
Kwa upande wake Kamishina Jenerali Lyimo amemshukuru Stive Nyerere kwa kufika ofisini kwao lakini pia kwa ujumbe mzuri ambao umewapatia kutoka kwa wasanii , na wao kama Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wanatambua msanii ni hazina.
Ameongeza msanii ndiye anayefanya Tanzania ifahamike, ijulikane na kwamba msanii ni hazina, msanii ni kioo cha jamii, hivyo ni lazima sasa hiyo hazina pengine kwa gharama zozote zile ilindwe.
Amefafanha inasikitisha unapoona msanii amekuwa kwa kipaji chake na uwezo wake anatoa nyimbo nzuri zinazotambulika mpaka kidunia lakini mwisho wa siku anaingia kwenye dawa za kulevya, anapotea, hivyo wanakuwa wamepoteza kipaji, wamepoteza hazina.
"Kwa hiyo jukumu la Mamlaka ni kulinda hivyo vipaji ambavyo ni hazina ili usanii uwe ni usaniii ambao unaleta hadhi kwa taifa , unaleta hadhi kwa serikali lakini hata viongozi wa serikali na serikali kwa ujumla inawatumia wasanii katika shughuli zake mbalimbali lakini wakiwa wanaheshimika na jamii pamoja na serikali
" Ndio maana tunataka kuanzia sasa hivi tunataka tuwatoe huko , kwa hiyo tunalinda hii hazina , sote twende kwa pamoja na wasaniii iwe ni kuelimisha jamii kweli , kuifanya jamii iondokane na maovu na kurudi kwenye hali halisi ,hali nzuri , hali yenye heshima , hali yenye maadili na ndicho wanachokijenga kama Mamlaka."
0 Comments