NAIBU Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) leo Disemba 15 2023, ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chujio la maji katika eneo la Mangamba na Uchimbaji wa visima vya maji eneo la Magomeni-Kagera Mkoani Mtwara.
Katika Ziara yake Mahundi amesema kuwa ujenzi wa chujio hilo lina uwezo wa kuchuja maji lita milioni 12 kwa siku ambapo limewezesha wakazi wa Mji wa Mtwara kupata huduma ya maji yaliyosafishwa na kutibiwa kwa viwango vinavyokubalika.
Aidha pamoja na mambo mengine Mhandisi Mahundi ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira-Mtwara (MTUWASA) wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa miundombinu inayotakiwa kwenye kisima kilichochimbwa eneo la Magomeni-Kagera ili kiweze kutumika na hatimaye kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo ya Chipuputa, Magomeni na mjini Mtwara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Mwanahamisi Munkunda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji kwenye mkoa huo
Ikumbukwe kuwa Mradi wa ujenzi wa chujio la maji ulikamilika mwezi septemba, 2022 kwa gharama ya shilingi bilioni 3.4 na kuweza kuzindulia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mwezi Septemba,2023.
0 Comments